-
Wanajeshi wa Nigeria wasiopungua 12 wameuliwa katika mapigano na kundi la ISWA
Dec 16, 2018 23:11Wanajeshi wa Nigeria wasiopungua 12 wameuliwa na makumi ya wengine hawajulikani walipo baada ya kukabiliana na wanamgambo waliojitenga na kundi la Boko Haram waitwao ISWA huko kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno. Hayo yameelezwa na duru za kijeshi za nchi hiyo.
-
Nigeria yaitimua UNICEF kwa tuhuma za kuwapa mafunzo majasusi wa Boko Haram
Dec 15, 2018 03:31Jeshi la Nigeria limesimamisha shughuli za Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) katika eneo la kaskazini mashariki kwa nchi, kwa tuhuma kuwa maafisa wake wanawapa mafunzo na kushirikiana na majasusi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Hraram.
-
HRW yataka kushtakiwa askari wanaowakandamiza Waislamu Nigeria
Dec 12, 2018 09:10Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa mwito wa kufunguliwa mashitaka wanajeshi wa Nigeria wanaowakandamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia.
-
Wanajeshi wawili wauawa katika shambulio la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria
Dec 10, 2018 03:19Maafisa usalama wa Nigeria wametangaza kuwa, shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram dhidi ya kambi moja ya jeshi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo limepelekea wanajeshi wawili kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
-
Homa ya Manjano yaua watu 9 nchini Nigeria
Dec 06, 2018 11:21Mripuko wa homa ya manjano nchini Nigeria umesababisha vifo vya watu tisa katika jimbo la Edo kusini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
-
Ulimwengu wa Spoti, Disemba 3
Dec 03, 2018 03:21Haya ni baadhi ya matukio ya spoti yaliyogonga vichwa vya habari ndani ya siku saba zilizopita, kitaifa na kimataifa....
-
Polisi ya Nigeria yaua 'majambazi' 100 jimboni Zamfara
Dec 01, 2018 04:38Polisi ya Nigeria imedai kuwa imefanikiwa kuwaangamiza majambazi 100 katika operesheni iliyofanyika katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa nchi.
-
Waislamu Nigeria waendelea kuandamana kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru
Nov 28, 2018 23:40Wananchi Waislamu wa Nigeria wamefanya maandamano ya kutaka kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky aachiliwe huru.
-
Boko Haram yawateka nyara watema kuni 50 Nigeria
Nov 23, 2018 04:26Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram limeripotiwa kuwateka nyara makumi ya watu waliokuwa wanatema kuni kaskazini mashariki mwa Nigeria, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.
-
Jeshi la Nigeria lakosolewa kwa 'kumuua mara mbili' kamanda wa Boko Haram
Nov 20, 2018 04:34Waandishi wa habari, wakosoaji wa serikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Nigeria wamelijia juu jeshi la nchi hiyo kwa kutangaza kuwa limemuua kamanda mwandamizi wa kundi la kigaidi la Boko Haram, licha ya kutoa taarifa kama hiyo mwaka jana.