-
Museveni aituhumu UN kuwa 'inalinda ugaidi' Kongo DR
Jan 17, 2018 11:14Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameibua tuhuma nzito dhidi ya Umoja wa Mataifa akidai kuwa chombo hicho cha kimataifa 'kinalinda ugaidi' mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Rais Assad: Matatizo ya Waarabu yanasababishwa na fikra potovu
Jan 16, 2018 01:16Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, matatizo yanayoukumba ulimwengu wa Kiarabu yanatokana na fikra potovu na kwamba madamu tatizo hilo halijatatuliwa, basi bado migogoro na vita vitaendelea kushuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Rais wa Tunisia afanya mkutano wa kusitisha maandamano
Jan 14, 2018 04:23Rais wa Tunisia amevunja kimya chake na kufanya mkutano na vyama vya siasa, miungano ya wafanyakazi na shirikisho la waajiri kwa shabaha yan kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa kiuchumi na maandamano yanayoshuhudiwa nchini humo kwa siku kadhaa sasa.
-
Upinzani Gabon wapinga kuondolewa kikomo cha mihula ya urais
Jan 13, 2018 00:14Vyama vya upinzani nchini Gabon vimepinga vikali hatua ya Bunge la nchi hiyo ya kuifanyia marekebisho katiba, kwa lengo la kumuondolea visiki njiani Rais Ali Bongo wa nchi hiyo ili aendelea kung'ang'ania madaraka.
-
Waliberia washiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais hii leo
Dec 26, 2017 04:04Wananchi wa Liberia wameelekea katika masanduku ya kupigia kura asubuhi ya leo kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
-
Makazi ya Rais Kabila wa DRC yateketezwa moto, polisi auawa
Dec 26, 2017 03:56Kundi la waasi wa Mai-Mai la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limevamia na kuteketeza moto nyumba ya Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
-
ICC yazijia juu nchi wanachama kwa kutomkamata Rais wa Sudan
Dec 13, 2017 23:42Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amezikosoa vikali baadhi ya nchi wanachama wa Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo, kwa kukataa kumtia mbaroni Rais Omar al-Bashir wa Sudan alipozitembelea.
-
Rais wa Msumbiji awapiga kalamu nyekundu mawaziri wanne
Dec 13, 2017 11:48Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amewafuta kazi mawaziri wanne wakiwemo wa mambo ya nje na mafuta. Hata hivyo ofisi yake haijatoa sababu ya kupigwa kalamu nyekundu mawaziri hao.
-
Uchunguzi wa maoni: Asilimia 85 ya Waganda 'hawamtaki' Museveni
Dec 10, 2017 03:44Uchunguzi wa maoni umeonyesha kuwa asilimia 85 ya wananchi wa Uganda hawaungi mkono muswada wa kufanyia marekebisho katiba ili kuondoa kikomo cha umri wa kugombea urais.
-
Mnangagwa ateua baraza la mawaziri, wanajeshi na wapambe wa Zanu-PF wafaidi
Dec 01, 2017 04:06Emmerson Mnangagwa, Rais mpya wa Zimbabwe ameteuwa baraza lake jipya la mawaziri, linalojumuisha maafisa wa ngazi za juu kwenye jeshi la nchi hiyo na viongozi 'waaminifu' wa chama tawala ZANU-PF.