-
Sudan yaafiki kuanzishwa nchini humo kambi ya jeshi la wanamaji la Russia
Feb 13, 2025 02:52Khartoum na Moscow zimekubaliana juu ya kuanzishwa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini Sudan.
-
Jibu la Russia kwa vitisho vya Trump dhidi ya BRICS
Feb 11, 2025 02:44Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa kuhusiana na tishio la Rais Donald Trump wa Marekani la kutoza ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za BRICS iwapo dola itafutwa katika mabadilishano ya kibiashara ya nchi hizo, na kusisitiza kuwa ushirikiano wa nchi wanachama wa BRICS unalenga kuimarisha uwezo wa kijamii, kiuchumi na kibinadamu wa nchi hizo.
-
DRC yawapandisha kizimbani wanajeshi wake kwa kutoroka vita; inawatuhumu pia kwa ubakaji
Feb 10, 2025 07:22Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa wanajeshi wasiopungua 75 wanatazamiwa kufikishwa mahakamani leo Jumatatu wakikabiliwa na shtaka la kuwakimbia wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika jimbo la Kivu ya Mashariki.
-
Moscow: Zelensky 'ana kichaa' kwa kutaka silaha za nyuklia za NATO
Feb 06, 2025 02:32Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amesema mwito wa Rais wa Ukraine, Vladimir Zelensky wa kutaka Kyev ipewe silaha za nyuklia na shirika la kijeshi la NATO unatia wasiwasi mkubwa.
-
Russia: Kwa mtazamo wa mkuu wa UNICEF watoto wa Ghaza si muhimu kama wenzao wa Ukraine
Jan 25, 2025 06:12Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amemshutumu mkuu wa UNICEF kwa kuwapa kipaumbele watoto wa Ukraine kuliko watoto wenzao wa Ghaza baada ya kushindwa kulieleza Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu masaibu ya watoto hao kama alivyofanya kwa watoto wa Ukraine.
-
Pezeshkian: Iran na Russia hazitakubali kuburuzwa na maadui
Jan 25, 2025 03:03Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa, mapatano kamili ya ushirikiano wa kistratejia kati ya Iran na Russia yanaonyesha kwamba Tehran na Moscow kamwe hazitakubali matakwa ya kupindukia ya maadui, akisisitiza kuwa nchi mbili hizi zitashirikiana kuunda sera zinazotoa kipaumbele kwa masuala ya utulivu, usalama, maendeleo na ustawi wa uchumi katika eneo.
-
Kutekelezwa Makubaliano ya Kifedha kati ya Iran na Russia
Jan 21, 2025 02:33Gavana wa Benki Kuu ya Iran, Mohammadreza Farzin, amesema kuwa kupitia utekelezaji wa makubaliano ya kifedha kati ya Iran na Russia, sarafu za mataifa haya mawili zitakuwa msingi wa biashara kati ya nchi hizo kwa mujibu wa kiwango cha mabadilishano kilichokubaliwa sokoni.
-
Araqchi: Asili ya makubaliano ya Iran na Russia ni ya kiuchumi
Jan 18, 2025 11:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya kina ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Iran na Russia yanahusu vipengee vyote vya uhusiano wa nchi na kwamba asili ya makubaliano hayo zaidi ni katika uga wa uchumi.
-
Russia yasisitiza umuhimu wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kistratejia na Iran
Jan 16, 2025 04:28Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin (makao makuu ya urais wa Russia), Jumanne alisema kuwa Russia inatilia umuhimu mkubwa kusainiwa mkataba wa ushirikiano wa kina wa kistratejia na Iran, akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu muhimu sana ya safari ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.
-
Maana ya ushirikiano mpya wa Iran na Russia kwa ulimwengu
Jan 10, 2025 12:44Chombo kimoja cha habari cha Russia kimetathmini ushirikiano wa Iran na Russia na kuandika: Makubaliano ya pamoja ya kistratejia ni hatua muhimu katika kuimarika muungano kati ya mataifa haya mawili.