-
Jeshi la Rwanda lakamata wanamgambo 19 wa Burundi mpakani
Oct 04, 2020 07:35Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limewatia mbaroni wanamgambo 19 wa Burundi waliokuwa wamejizatiti kwa silaha katika mpaka wa nchi mbili hizo jirani.
-
Rusesabagina asema alihadaiwa na kupelekwa Rwanda badala ya Burundi
Sep 18, 2020 10:41Paul Rusesabagina anayejulukana kama Shujaa wa filamu ya 'Hotel Rwanda' inayosimulia kisa cha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, anasema kuwa, aliamini alikuwa akisafiri kwenda Burundi kwa mwaliko wa mchungaji wa kanisa, lakini badala yake akahadaiwa na kupelekwa Rwanda na kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi.
-
Shujaa wa filamu ya 'Hotel Rwanda' afikishwa mahakamani kwa makosa ya ugaidi, mauaji
Sep 14, 2020 11:27Shujaa wa filamu ya 'Hotel Rwanda' inayosimulia kisa cha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, Paul Rusesabagina, leo Jumatatu amefikishwa mahakamani mjini kigali akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi, kufadhili ugaidi mauaji na kuteka nyara.
-
Sherehe za harusi zaruhusiwa Rwanda, lakini...
Sep 07, 2020 15:40Wizara ya serikali za mitaa nchini Rwanda imetangaza masharti mapya kwa watu wanaojiandaa kufunga pingu za maisha kwa kuwataka watu watakaohudhuria harusi zao wawe wamepima corona kwa muda wa saa 72 zilizopita kabla ya harusi yenyewe. Hata hivyo gharaza upimaji zitakuwa dola 50 kwa kila mtu mmoja kitu ambacho wananchi wamekilalamikia. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
-
Kundi la kwanza la wakimbizi wa Burundi larejea nyumbani kutoka Rwanda
Aug 28, 2020 02:23Mamia ya wakimbizi raia wa Burundi walioko nchini Rwanda wameanza kurejea nchini kwao, miaka mitano baada ya kukimbia mapigano na ghasia za kisiasa.
-
Rwanda yatoa waranti wa kumtia mbaroni mshukiwa wa mauaji ya kimbari aliyeko Ufaransa
Aug 27, 2020 04:05Rwanda imetoa waranti wa kumtia mbaroni Aloys Ntiwiragabo Mkuu wa zamani wa Intelijinsia wa nchi hiyo ambaye yuko chini ya uchunguzi hivi sasa nchini Ufaransa kwa kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 huko Rwanda.
-
Makaburi mawili ya umati yapatikana kandokando ya mji mkuu wa Rwanda
Aug 18, 2020 14:57Mabaki ya makumi ya miili ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda dhidi ya Watutsi yamepatikana katika wilaya ya Nyarugenge kandokando ya mji mkuu wa Rwanda, Kigali.
-
Rwanda: Serikali imetumia dola milioni 60 kukabiliana na Covid-19
Jul 21, 2020 10:54Wizara ya Afya ya Rwanda imesema kuwa serikali imetumia dola za Kimarekani milioni 60 ambazo ni zaidi ya faranga za nchi hiyo bilioni 54 katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 tangu kuthibitishwa kesi ya kwanza ya ugonjwa huo nchini humo.
-
Rwanda yasikitishwa na mauaji ya askari wake Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jul 16, 2020 08:07Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limeeleza kusikitishwa kwake na mauaji ya askari wa kulinda amani wa nchi hiyo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
EABC yazitaka nchi zote za Afrika Mashariki kufungua anga zao, kuruhusu utalii na biashara
Jul 14, 2020 13:08Baraza la Biashara la Nchi za Afrika Mashariki (EABC), limezisihi nchi zote za kanda hiyo kufuata mfano wa Tanzania kwa kufungua anga zao ili kuruhusu safari za kimataifa kuingia na kutoka katika nchi zote za kanda hiyo.