-
Sekta ya usafiri Uganda yalalamikia kubanwa mno wakati wa corona
Oct 02, 2020 18:37Serikali ya Uganda imezidi kupunguza masharti yanayohusiana na ugonjwa wa COVID-19 lakini pamoja na hayo, sekta ya usafiri imekumbwa na changamoto nyingi. Mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail, na maelezo zaidi.
-
Sala za Ijumaa zaanza upya nchini Uganda + Sauti
Sep 26, 2020 05:00Sala za Ijumaa zimeanza tena nchini Uganda baada ya kusimamishwa kwa muda kutokana na maambukizi ya kirusi cha corona. Katika hotuba za jana Ijumaa, Waislamu nchini humo walihimizwa kumtii Mola Karima na kuomba kusamehewa madhambi yao. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala.
-
Sherehe za harusi zaruhusiwa Rwanda, lakini...
Sep 07, 2020 15:40Wizara ya serikali za mitaa nchini Rwanda imetangaza masharti mapya kwa watu wanaojiandaa kufunga pingu za maisha kwa kuwataka watu watakaohudhuria harusi zao wawe wamepima corona kwa muda wa saa 72 zilizopita kabla ya harusi yenyewe. Hata hivyo gharaza upimaji zitakuwa dola 50 kwa kila mtu mmoja kitu ambacho wananchi wamekilalamikia. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
-
Wapinzani Uganda walalamikia kukandamizwa wakati huu wa kukaribia uchaguzi mkuu + Sauti
Jul 14, 2020 06:17Ikiwa imebakia miezi saba hadi kufanyika Uchaguzi Mkuu nchini Uganda, wanasiasa wa vyama mbalimbali nchini humo wanawalalamikia askari wa kulinda usalama kwa kuwakandamiza. Taarifa zaidi anayo mwandishi wetu Kigozi Ismail kutoka Kampala
-
Spika wa zamani wa Gabon aanzisha kampeni ya kupinga kuhalalishwa ngono za jinsia moja + Sauti
Jul 14, 2020 02:36Spika Mstaafu wa Bunge la Gabon ameanzisha kampeni za kupinga sheria iliyopasishwa bungeni hivi karibuni ya kuhalalisha vitendo haramu vya kulawitiana na ngono za watu wa jinsia moja nchni humo. Amesema kuwa vitendo hivyo ni kinyume na mila na desturi za watu wa Gabon. Maelezo zaidi anayo mwandishi wetu, Mossi Mwasi kutoka Brazzaville.
-
DRC inasherehekea miaka 60 ya uhuru hali ikiwa bado mbaya + Sauti
Jul 01, 2020 07:45Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasherehekea miaka 60 wa uhuru wake kutoka kwa mkonoloji wa Ulaya, Ubelgiji, huku hali ya amani na uchumi ikiwa bado ni mbaya sawa kabisa na ilivyokuwa muda mchache tu baada ya kujipatia uhuru huo. Mossi Mwassi na maelezo zaidi kutoka Brazzaville.
-
Baraza jipya la Mawaziri lala kiapo nchini Burundi + Sauti
Jul 01, 2020 07:42Baraza jipya la mawaziri wa serikali ya Burundi lilikula kiapo jana Jumanne mbele ya rais na mabaraza ya bunge na seneti. Chama kikuu cha upinzani cha CNL hakijashirikishwa katika serikali hiyo. Hamida Issa na malezo zaidi kutoka Bujumbura na maelezo zaidi.
-
Wazayuni wafanya ufisadi mkubwa nchini Cameroon + Sauti
Jun 26, 2020 16:49Rais Paul Biya wa Cameruni ameganda madararakani miaka nenda miaka rudi kwa msaada wa mamluki wa Kiyahudi ambao sasa wanalaumiwa kwa kuua watu wengi na pia kwa kupora mali ya uma nchini humo. Hayo ni matokeo ya uchunguzi wa waandishi wa habari wawili chini ya taasisi ya kupiga vita rushwa nchini humo. Mosi Mwasi na maelezo zaidi kutoka Brazaville
-
Uganda yaanza zoezi la kuwarejesha nyumbani wananchi waliokwamishwa na corona + Sauti
Jun 24, 2020 15:34Serikali ya Uganda imeanza kutekeleza zoezi la kuwarejesha nyumbani wananchi wa nchi hiyo waliokwama katika nchi za ndani na nje ya Afrika kutokana na kuenea ugonjwa wa COVID-19. Serikali ya Uganda imepanga kuwaweka kwenye karantini watu wote wanaorejea nchini humo. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala
-
Serikali ya Burundi yatoa tamko rasmi la kufariki dunia rais wa nchi hiyo + Sauti
Jun 10, 2020 16:07Serikali ya Burundi imetangaza rasmi kifo cha rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ambaye ameiongoza Burundi kwa muda wa miaka 15. Serikali ya Bujumbura imetangaza siku 7 za maombolezo ya kitaifa na bendera ya nchi hiyo itapepea nusu mlingoti.