-
Evariste Ndayishimiye rais mpya wa Burundi + Sauti
May 26, 2020 02:20Tume ya uchaguzi ya Burundi, jana Jumapili ilimtangaza Evariste Ndayishimie kuwa rais mpya wa nchi hiyo huku ishara zote zikiwa zimeonesha tangu awali kabisa kwamba mgombea huyo wa chama tawala angelitangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais.
-
Zanzibar kupunguza marufuku za kukabiliana na COVID-19
May 24, 2020 17:08Serikali ya Zanzibar SMZ imesema imekusudia kupunguza masharti iliyokuwa imeyaweka hapo kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit na maelezo zaidi.
-
Hatimaye serikali ya Kenya yapambana na corona kwa kufunga kikamilifu maeneo ya Nairobi na Mombasa + Sauti
May 06, 2020 16:07Hatimaye serikali ya Kenya imeamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuifungia kikamilifu baadhi ya mitaa ya Nairobi na Mombasa kwa muda wa siku 15 kutokana na ukaidi wa baadhi ya watu wasioheshimu maagizo ya maafisa wa afya.
-
Msalaba Mwekundu yaomba msaada wa kupambana na corona CAR + Sauti
Apr 15, 2020 17:55Shirika la Msalaba Mwekundu Jamhuri ya Afrika ya Kati limeyaomba mataifa ya dunia yalisaidie shirika hilo kupambana na maambukizi ya corona nchini humo. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
Licha ya kupita miaka 26 ya mauaji ya kimbari Rwanda, bado athari zake zingalipo + Sauti
Apr 09, 2020 13:13Wakati Rwanda ikiendelea kuomboloza mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Watutsi ya mwaka 1994, bado kuna walionusurika na mauaji ambao wanaendelea kuishi na msongo wa mawazo kutokana na athari za mauaji hayo. Sylvanus Karemera na maelezo zaidi kutoka Kigali.
-
Tume ya Uchaguzi Burundi CENI yakutana na wapiga kura wa jamii ya mbilikimo + Sauti
Feb 18, 2020 11:22Tume ya Uchaguzi Burundi CENI, imekutana na wajumbe wa mashirika ya kiraia ya watu wajamii ya mbilikimo ili kuwahamasisha wateue wagombea watakaowawakilisha katika uchaguzi wa bunge na seneti. Ceni imewaongezea mbilikimo hao muda wa siku 5 kwenye kalenda ya siku zilopangwa za kuhakikisha zoezi hilo limekamilika. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Burujumbura Burundi
-
Wilaya nyingine 15 zavamiwa na nzige nchini Uganda + Sauti
Feb 18, 2020 11:17Janga la nzige limezidi kuwa tishio barani Afrika huku wizara ya kushughulikia majanga nchini Uganda ikisema kuwa, wilaya nyingine 15 zimevamiwa na wadudu hao nchini humo. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala
-
Kagame: Siwezi kuwavumilia wezi na watu wasio na nidhamu serikalini + Sauti
Feb 18, 2020 11:13Wiki moja baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake watatu, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kwa mara nyingine tena kwamba hatavumilia hata kidogo viongozi wasio na nidhamu katika serikali yake. Ndani ya wiki moja tu Rais Paul Kagame amewafuta mawaziri watatu kutokana na makosa ya ulaji rushwa, udanganyifu pamoja na ukosefu wa nidhamu mbele ya wananchi. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi
-
UN yaumizwa na mauaji ya kiholela nchini Cameroon + Sauti
Feb 18, 2020 11:01Umoja wa Mataifa na asasi za kijamii nchini Cameroon zimeelezea kusikitishwa na mauaji ya kiholela ya watu zaidi ya 25 ambao taarifa zinasema kwamba wameuliwa nchini humo na watu waliokuwa wamevaa magwanda ya kijeshi. Mossi Mwasi na maelezo zaidi
-
Waislamu Kenya waadhimisha Siku ya Vazi la Hijab Duniani + Sauti
Feb 01, 2020 15:47Vyama vya Kiislamu nchini Kenya vimehimizwa kushadidisha hamasa juu ya vazi la hijab miongoni mwa Waislamu kama njia pekee ya kukinusuru kizazi cha Kiislamu dhidi ya sheria dhalimu zinazomkandamiza binti wa Kiislamu. Mwito huo umetolewa sanjari na maadhimisho ya Siku ya Vazi la Hijab Duniani ambayo huadhimishwa Februari Mosi kila mwaka. Seifullah Muurtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.