Kagame: Siwezi kuwavumilia wezi na watu wasio na nidhamu serikalini + Sauti
Feb 18, 2020 11:13 UTC
Wiki moja baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake watatu, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kwa mara nyingine tena kwamba hatavumilia hata kidogo viongozi wasio na nidhamu katika serikali yake. Ndani ya wiki moja tu Rais Paul Kagame amewafuta mawaziri watatu kutokana na makosa ya ulaji rushwa, udanganyifu pamoja na ukosefu wa nidhamu mbele ya wananchi. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi
Tags