-
Sudan Kusini yawaachia huru msemaji na mshauri wa kiongozi wa waasi
Nov 02, 2018 12:36Sudan Kusini leo imewaachia huru kutoka jela msemaji na mshauri wa Riek Machar kiongozi wa waasi wa nchi hiyo. Hayo yameelezwa na afisa wa serikali ya Juba.
-
Kiongozi wa waasi Sudan Kusini arejea nchini baada ya kufikiwa makubaliano ya amani
Oct 31, 2018 12:13Riek Machar kiongozi wa waasi Sudan Kusini leo Jumatano amewasili Juba mji mkuu wa nchi hiyo kuadhimisha makubaliano ya amani; ikiwa imepita zaidi ya miaka miwili baada ya kuibuka mapigano makali huko Juba na kumlazimisha kukimbia nchi.
-
UN: Machafuko ya Sudan Kusini yanazuia ugawaji wa misaada ya chakula
Oct 29, 2018 11:00Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kuwa, machafuko yanayoendelea nchini Sudan Kusini yanazuia operesheni za kugawa misaada ya chakula kwa watu wanaosumbuliwa na njaa kali katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
-
UN: Pande hasimu Sudan Kusini ziliwateka nyara na kuwanajisi mamia ya wanawake
Oct 24, 2018 13:19Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umeeleza kuwa, askari wa serikali na waasi nchini humo wamewateka nyara mamia ya wanawake na wasichana mwaka huu na wengi miongoni mwao walibakwa na kufanywa watumwa wa ngono.
-
Wapinzani wa serikali ya Sudan Kusini wahusishwa na jinai dhidi ya wanawake na watoto
Oct 19, 2018 11:13Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, wapinzani wenye silaha nchini Sudan Kusini wamekuwa wakiwabaka na wakuwadhalilisha kijinsia wasichana na wanawake, baada ya kuwateka.
-
UN yaongeza 'muda wa mwisho' wa kuhudumu kikosi chake Abyei
Oct 12, 2018 04:00Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kuongezewa muda wa kuhudumu kikosi chake cha kulinda amani katika eneo la Abyei, lililoko kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini.
-
Wafungwa Sudan Kusini wadhibiti seli katika mji mkuu Juba
Oct 07, 2018 23:04Wafungwa kadhaa jana Jumapili waliwapokonya silaha walinzi na kisha kudhibiti eneo moja la seli ya wafungwa huko Juba mji mkuu wa Sudan Kusini. Hayo yameelezwa na Idara ya Usalama wa taifa ya nchi hiyo.
-
Wafungwa wazusha ghasia Sudan Kusini, waiba silaha
Oct 07, 2018 04:13Hali ya taharuki imetanda katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, baada ya mamia ya wafungwa katika gereza moja kuvunja ghala la silaha na kukabiliana na walinzi.
-
Sudan Kusini yaiambia UN kuwa makubaliano ya amani hayatakiukwa
Sep 29, 2018 04:46Makamu wa Rais wa Sudan Kusini ameuambia mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba makubaliano ya amani ya mara hii yaliyofikiwa hivi karibuni na mahasimu wa kisiasa wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika yatadumu na wana wingi wa matumaini kwamba hayatakiukwa.
-
Ripoti: Mapigano nchini Sudan Kusini yameua watu laki 4
Sep 26, 2018 10:16Ripoti mpya inasema watu karibu laki nne wameuawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan Kusini.