-
Araghchi: Matukio ya Syria ni sehemu ya njama za Wamarekani na Wazayuni dhidi ya eneo
Dec 02, 2024 07:23Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo yake na Rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Damascus, kwamba matukio ya Syria ni sehemu ya njama za Wazayuni na Wamarekani dhidi ya eneo la Asia Magharibi.
-
Kanani: Kuwekewa vikwazo ndege za Iran ni ugaidi wa kiuchumi wa nchi za Magharibi
Sep 11, 2024 07:07Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameichukulia kauli ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusiana na kufutwa makubaliano ya pande mbili ya kutoa huduma za anga kwa Iran kuwa ni ugaidi wa kiuchumi wa nchi za Magharibi dhidi ya taifa la Iran.
-
Iran: Uingereza inaendeleza siasa za kindumilakuwili kuhusu ugaidi
Aug 31, 2024 04:16Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London umeilaumu Uingereza kwa siasa zake za nyuso mbili kuhusu ugaidi na kusema kuwa, wakati wananchi wa Iran wanapouawa kigaidi, kwa mujibu wa serikali ya London, ugaidi huo unavumilika, na hauwezi kuchukuliwa msimamo kama wa ugaidi unaofanyika maeneo mengine.
-
Gharibabadi: Nchi za Magharibi ziache sera za kinafiki na ubaguzi kuhusiana na ugaidi
Apr 18, 2024 13:35Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema kuwa, Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinapaswa kuachana na siasa zao za kindumakuwili na ubaguzi kuhusiana na ugaidi.
-
Shambulizi la Moscow... Russia yaitaka Kiev kumkabidhi mkuu wa usalama
Apr 01, 2024 10:43Russia imeitaka Ukraine kuwakabidhi raia wake kadhaa, akiwemo Mkuu wa Idara ya Usalama ya nchi hiyo, kwa madai kwamba walihusika na vitendo vya "kigaidi" katika ardhi ya Russia, suala ambalo Kiev imelitaja kuwa takwa"lisilo na thamani".
-
Axios: Netanyahu atasusiwa na sehemu kubwa ya wawakilishi wa Congress
Mar 22, 2024 06:59Tovuti ya habari ya Marekani ya Axios imesema kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, huenda akasusiwa pakubwa na "wabunge wa Congress ikiwa atakubali mwaliko wa kuzungumza mbele ya Bunge la Marekani.
-
Mahakama ya Misri yamhukumu kifo kiongozi wa Ikhwanul Muslimin na wenzake 7
Mar 05, 2024 07:40Mahakama ya Misri imemhukumu kifo kiongozi wa chama cha Ikwanul Muslimin (Muslim Brotherhood), Mohamed Badie, na viongozi wengine saba wa harakati hiyo baada ya kuwatia hatiani kwa eti kupanga vitendo vya ukatili kwa "madhumuni ya kigaidi" wakati wa mgomo wa Cairo mwaka 2013.
-
UN: Tishio la ugaidi ni kubwa katika maeneo yenye mizozo Afrika na Afghanistan
Feb 03, 2024 12:42Tishio la ugaidi la mtandao wa kigaidi na kitakfiri wa al Qaida, kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) na makundi mengine yenye mfungamano na magenge hayo lingali kubwa katika maeneo yenye migogoro barani Afrika na huko Afghanistan, na viwango cha vitisho vinaongezeka katika baadhi ya maeneo ikiwemo barani Ulaya.
-
Azma thabiti ya Iran na Pakistan ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Jan 20, 2024 03:00Baada ya kushadidi mivutano ya mpakani kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan katika kipindi cha siku mbili zilizopita, viongozi wa Tehran na Islamabad wamesisitiza kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, kuheshimiwa umoja wa ardhi za mataifa hayo mawili na kuwepo uratibu na mashauriano ya karibu zaidi katika kupambana na magenge ya kigaidi.
-
Hatua za undumakuwili za nchi za Ulaya kuhusu ugaidi
Jan 14, 2024 02:43Mahakama ya Rufaa ya Denmark inayojulikana kwa jina la "The Eastern High Court" Ijumaa tarehe 12 Januari ilipasisha hukumu ya kifungo jela kwa watu watatu ambao ni wanachama wa kundi linalotaka kujitenga la "Al Ahwaziya" ambao walituhumiwa kueneza ugaidi nchini na kukusanya taarifa za kijasusi kwa ajii ya Shirika la ujasusi la Saudi Arabia.