Apr 18, 2024 13:35 UTC
  • Kazem Gharibabadi
    Kazem Gharibabadi

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema kuwa, Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinapaswa kuachana na siasa zao za kindumakuwili na ubaguzi kuhusiana na ugaidi.

Kazem Gharibabadi ameyasema hayo akiwa nchini Syria alikokwenda kushiriki katika kikao cha kwanza cha kamati ya pande tatu cha Mahakama ya Iran, Iraq na Syria ili kukabiliana na ugaidi.

Gharibabadi, amesema kuwa Iran, Iraq na Syria ni wahanga wa ugaidi na hujuma za kigaidi na kueleza kuwa, maadui na kambi ya ubeberu, wameshindwa kusogeza mbele njama na mipango yao licha ya kuunganishwa pamoja uwezo na nguvu zao.

Kazem Gharibabadi

Akiashiria operesheni "Ahadi ya Kweli" ya kuuadhibu utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel baada ya kushambulia ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria, Gharibabadi ameongeza kuwa, jibu la Iran kwa utawala wa Kizayuni limetolewa kwa mujibu wa kanuni za Hati ya Umoja wa Mataifa na ndani ya fremu ya haki halali ya kujilinda.

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema, inasikitisha kuona kuwa, badala ya kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, nchi za Magharibi na Marekani zinaendelea kuuunga mkono utawala huo unaofanya mauaji ya kimbari.

Tags