-
9 wafariki, wakiwemo watoto 6 katika msongamano wa mkesha wa mwaka mpya Uganda
Jan 02, 2023 03:44Watu wasiopungua tisa wamefariki dunia wakiwemo vijana wadogo sita katika msongamano uliotokea wakati wa sherehe za mkesha wa mwaka mpya katika duka kuu moja la mji mkuu wa Uganda, Kampala.
-
Mafuriko yaua watu 10 kusini mwa Uganda, mamia walazimishwa kuhama makazi yao
Dec 28, 2022 00:51Maafisa wa serikali ya Uganda wametangaza kuwa mafuriko yaliyotokea jana kusini mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 10.
-
ICC yathibitisha adhabu ya kifungo cha miaka 25 jela aliyopewa 'aliyekuwa askari mtoto' wa LRA ya Uganda
Dec 16, 2022 08:29Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetupilia mbali rufaa ya Dominic Ongwen, raia wa Uganda aliyegeuzwa kamanda wa kijeshi akiwa mtoto mdogo katika kundi la waasi la Lord's Resistance Army (LRA), aliyepinga adhabu aliyopewa baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
-
Wapiganaji 15 wa ADF wauawa na jeshi la Uganda mpakani na DRC
Dec 14, 2022 07:57Askari wa Jeshi la Uganda wamefanikiwa kuwaangamiza wanamgambo 15 wa kundi la waasi la ADF katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wanandoa wa Marekani waswekwa rumande Uganda kwa kumtesa mtoto wa miaka 10
Dec 13, 2022 04:02Mke na mume raia wa Marekani wanaoishi katika mtaa wa Naguru huko Kampala, mji mkuu wa Uganda wametupwa rumande katika gereza la Luzira, wakikabiliwa na mashitaka ya kumtesa na kumdhalilisha mtoto mdogo wa miaka 10.
-
Waziri: Ukimwi unaua Waganda 46 kila siku
Nov 30, 2022 07:28Waziri katika Ofisi ya Rais nchini Uganda ameashiria ongezeko la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa tabaka la vijana wanaobaleghe nchini humo na kusema kuwa, maradhi hayo yanaua Waganda 46 kwa siku.
-
Uganda kutuma askari 1,000 DRC kuwa sehemu ya kikosi cha kieneo
Nov 22, 2022 00:01Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) limesema litatuma mamia ya askari wake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujiunga na kikosi cha kieneo kinachopambana na magenge ya waasi na wabeba silaha mashariki mwa DRC.
-
Uganda yanakili kesi ya kwanza ya Ebola eneo la mashariki
Nov 13, 2022 10:11Kesi ya ugonjwa wa Ebola imethibitishwa kutokea mjini Jinja kusini mwa Uganda, hiyo ikiwa ni kesi ya kwanza kuripotiwa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Afrika CDC: Mlipuko wa Ebola nchini Uganda "unadhibitika"
Oct 27, 2022 09:30Shirika la juu zaidi la afya ya umma barani Afrika (Afrika CDC) limetangaza leo Alhamisi kwamba mlipuko wa Ebola nchini Uganda bado unadhibitiwa, licha ya kuongezeka kwa kesi za maambukizi ya ugonjwa huo hadi katika mji mkuu, Kampala.
-
Mawaziri wa Uganda waanza kujifunza Kiswahili
Oct 27, 2022 04:34Mawaziri wa Uganda wameazimia kuanza kujifundisha lugha ya Kiswahili, ambayo mbali na kuwa lugha ya kitaifa, lakini pia ni lugha rasmi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.