-
Wayemen wafanya maandamano kulaani jinai za Wazayuni Gaza
Dec 15, 2023 10:17Wananchi wa Yemen kwa mara nyingine tena wamefanya maandamano makubwa ya kulaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na vile vile kuonyesha mshikamano wao na taifa la Palestina.
-
Iran na Saudia zataka vita dhidi ya Gaza visitishwe mara moja
Dec 13, 2023 12:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Saudi Arabia wamesisitizia udharura wa kusimamishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza haraka iwezekanavyo, sambamba na kutaka kufikishwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la Palestina lililo chini ya mzingiro.
-
Israel iliidondoshea Gaza mabomu 22,000 ya US ndani ya wiki 6
Dec 13, 2023 02:47Ripoti mpya imefichua kuwa, utawala haramu wa Israel ulidondosha zaidi ya mabomu 22,000 uliopewa na Marekani katika Ukanda wa Gaza, katika kipindi cha wiki sita za kwanza za mashambulizi ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa ukanda huo.
-
Israel yashambulia kwa mabomu shule 2 Gaza, 50 wauawa shahidi
Dec 05, 2023 06:54Vikosi vya utawala haramu wa Israel vimeshambulia kwa mabomu shule mbili katika Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina.
-
Mashirika ya haki Palestina yaonya kuhusu 'Nakba ya Pili' Gaza
Dec 05, 2023 06:52Mashirika matatu ya kutetea haki za binadamu ya Palestina yameashiria hatua ya Israel ya kuwafukuza kwa umati Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kuwa, utawala huo wa Kizayuni unapanga kukariri Nakba ya pili katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Piga nikupige baada ya usitisjai vita wa muda katika Ukanda wa Ghaza
Dec 04, 2023 07:27Hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushambulia kinyama kambi ya wakimbizi ya Jabalia katika Ukanda wa Ghaza kwa kutumia mabomu ya fosforasi na sambamba na kutumwa mabomu mapya kutoka Marekani kwa utawala huo ghasibu ni miongoni mwa matukio ya hivi karibuni kuhusiana na Palestina.
-
Askari 60 wa Kizayuni waangamizwa katika operesheni ya HAMAS
Dec 03, 2023 10:43Makumi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameangamizwa katika operesheni ya Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu HAMAS.
-
Amir-Abdollahian: Uwepo wa dola la Kizayuni umeitia kwenye matatizo makubwa dunia
Dec 02, 2023 10:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza zimeiweka kwenye alama ya kuuliza itibari ya jamii ya kimataifa na madai ya kupigania haki za binadamu ulimwenguni.
-
Yemen: Silaha zetu zitaendelea kuupiga utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 02, 2023 10:42Mjumbe wa ngazi za juu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, silaha za nchi yake zimeelekezwa kwa adui Mzayuni ambaye ndiye adui nambari moja na kwamba utaendelea kuzitumia silaha hizo kuupiga utawala huo dhalimu.
-
Israel yaanza tena kumwaga damu za Wapalestina Gaza, makumi wauawa shahidi
Dec 01, 2023 07:55Miripuko kadhaa na milio ya risasi imesikika kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya utawala haramu wa Israel kuanzisha tena hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu, baada ya muda wa usitishaji vita kumalizika mapema leo.