-
Zarif: Iran itaishtaki Marekani Umoja wa Mataifa
Dec 17, 2017 00:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu itayawasilisha Umoja wa Mataifa madai ya Nikki Haley, balozi wa Marekani katika umoja huo kwamba eti Iran imeipatia silaha harakati ya Ansarullah ya Yemen.
-
UN: Kombora lililovurumishwa Riyadh Saudi Arabia si la Iran
Dec 15, 2017 00:47Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo amesisitiza kuwa, hakuna ushahidi wowote unaoweza kuthibitisha madai kwamba makombora yanayotumiwa na jeshi la Yemen kuipiga Saudi Arabia yanatoka nchini Iran.
-
Mjumbe wa UN: Wanawake Waislamu wa Myanmar wanabakwa hadi kufa
Dec 13, 2017 23:41Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu ukatili wa kingono unaofanywa na jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya na kutoa wito wa kutolewa azimio la Baraza la Usalama la kusitishwa ukatili huo mara moja.
-
UN: Watu zaidi ya milioni 8.4 wa Yemen wapo katika ncha ya kufa njaa
Dec 12, 2017 04:40Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, watu milioni 8 na laki 4 wamebakisha 'hatua moja' watumbukie katika mgogoro mkubwa njaa.
-
UN yaeleza wasiwasi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Libya
Dec 11, 2017 10:13Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika nchini humo.
-
Jumatatu 11 Disemba, 2017
Dec 11, 2017 00:05Leo ni Jumatatu tarehe 22 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1439 Hijria mwafaka na tarehe 11 Disemba mwaka 2017.
-
Jeshi la DRC laahidi kutoa jibu kali kwa waasi wa ADF baada ya kuua wasimamia amani
Dec 10, 2017 11:01Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeatangaza kuwa, litatoa jibu kali kwa mauaji yaliyofanywa na waasi wa ADF-NALU wa Uganda dhidi ya askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO.
-
Guterres: Mauaji dhidi ya askari wa UN huko Kongo ni 'jinai ya kivita'
Dec 09, 2017 03:45Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali mauaji ya wanajeshi wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO, na kuutaja ukatili huo kama jinai ya kivita.
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu ukame na njaa Sudan Kusini
Dec 08, 2017 23:03Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu ametahadharisha kuhusiana na kuzidi kuwa mbaya hali ya chakula kwa zaidi ya watu milioni moja huko Sudan Kusini.
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu kuteswa raia Cameroon
Dec 08, 2017 00:54Kamati ya Kukabiliana na Mateso ya Umoja wa Mataifa imetahadharisha kuhusu vitendo vya utesaji vinavyofanywa na wanajeshi wa serikali ya Cameroon dhidi ya raia chini ya anuani ya mapambano dhidi ya ugaidi katika maeneo ya wakazi wanaozungumza lugha ya Kiingereza.