-
Iran yaipongeza IAEA kwa kukiri kuwa Israel ina silaha za nyuklia, yataka ilazimishwe kuharibu silaha hizo
Dec 13, 2024 03:41Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kimataifa na Kisheria amejibu hatua ya kukiri Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu hatari za silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni, na kuutaka wakala huo ushughulikie silaha za nyuklia za Israel na sio kuusakama mradi wa matumizi ya amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ireland yajiunga na kesi ya Afrika Kusini ICJ dhidi ya Israel
Dec 13, 2024 03:40Serikali ya Ireland imetangaza kujiunga na kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala haramu wa Israel unaotenda jinai dhidi ya Wapalestina.
-
Ripoti: Wapalestina 4000 wameuawa kaskazini mwa Gaza katika kipindi cha miezi miwili
Dec 13, 2024 03:39Kwa akali Wapalestina 4000 wameuawa shahidi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza katika kipindi cha miezi miwili iliyopita kufuatia hatua za kikatili na hujuma za jeshi la utawala ghasibu wa Israel katika maeneo hayo.
-
RSF: Waandishi 54 wameuawa mwaka huu wakiwa kazini
Dec 13, 2024 03:38Shirika la kimataifa la Waandishi Habari wasiokuwa na Mipaka, RSF limetangaza kuwa, takribani waandishi habari 54 wameuawa ulimwenguni kote mwaka huu katika mazingira yanayohusisha kazi zao.
-
Reuters: Trump amemwambia Zelensky anataka vita "visimamishwe mara moja"
Dec 12, 2024 10:32Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemwambia Rais Vladimir Zelensky wa Ukraine na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwamba anataka kukomeshwa uhasama wa vita kati ya Russia na Ukraine haraka iwezekanavyo. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters likizinukuu duru kadhaa.
-
Israel yaishambulia Hospitali Ghaza mara kadhaa, yaua watu 30 kati ya waliokuwemo ndani
Dec 06, 2024 13:53Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeshambulia mara kadhaa hospitali ya Kamal Adwan na majengo kadhaa ya karibu ya makazi ya raia kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza, na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 30 na kuwajeruhi wengine wengi.
-
Sheikh Naim Qassim: Muqawama uko imara na umepata ushindi
Dec 06, 2024 03:51Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, muqawama ukitegemea nguvu na uwezo wa wapiganaji wake umepata ushindi katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Utawala wa Kizayuni wakiri kupata hasara kubwa kufuatia mashambulizi ya Hizbullah
Dec 04, 2024 12:18Mkuu wa kitongoji kimoja cha Wazayuni ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya nyumba ndani ya kitongoji hicho zimeharibiwa na kubomoka kufuatia mashambulizi ya makombora ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
-
Nandi-Ndaitwah atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi na kuwa rais wa kwanza mwanamke Namibia
Dec 04, 2024 06:39Namibia imepata rais wake wa kwanza mwanamke baada ya mgombea wa chama tawala cha SWAPO na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Bi Netumbo Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72, kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika wiki iliyopita.
-
Waziri wa Algeria atoka nje ya mkutano India kulalamikia kuwepo waziri wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 04, 2024 06:05Ujumbe wa Algeria, ukiongozwa na Waziri wake wa Biashara Tayeb Zitouni, umetuma salamu za kijasiri na za kivitendo katika Mkutano wa Ushirikiano (Patnership Summit) uliofanyika New Delhi, India kwa kutoka nje ya ukumbi mara baada ya kuwasili waziri wa uchumi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.