Sheikh Naim Qassim: Muqawama uko imara na umepata ushindi
(last modified Fri, 06 Dec 2024 03:51:24 GMT )
Dec 06, 2024 03:51 UTC
  • Sheikh Naim Qassim: Muqawama uko imara na umepata ushindi

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, muqawama ukitegemea nguvu na uwezo wa wapiganaji wake umepata ushindi katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Naim Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, adui Mzayuni alijaribu kuangamiza muqawama kupitia uvamizi wa kikatili wa Lebanon, lakini muqawama huo umesimama kidete mbele ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon sambamba na kueleza kuwa muqawama unaunga mkono umoja wa ardhi ya Lebanon na umoja wa kitaifa amebainisha kuwa Hizbullah inaendelea kusimama dhidi dhidi ya dhulma  na upendaji mkuu wa Israel.

Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassim amesema pia kuwa, uadui dhidi ya Syria unaofadhiliwa na Marekani na Israel, unafanya njama za kufikia malengo yake kwa kuiharibu Syria baada ya kushindwa huko Gaza na baada ya makubaliano kukomesha uchokozi dhidi ya Lebanon.

Amesisitiza kuwa, Hizbullahh itakuwa pamoja na Syria kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya kukwamisha malengo ya maaadui.