Gavana wa Darfur: Al Burhan aamuru vikosi kusonga mbele kuelekea magharibi
-
Jeshi la Sudan
Gavana wa Darfur na kiongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan, Minni Arko Minnawi amesema kwamba mkuu wa Baraza la Utawala na kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameamuru kusonga mbele kuelekea magharibi mwa Darfur.
Akihutubia vikosi vya jeshi huko Khartoum, Minnawi ameapa kuelekea magharibi mwa nchi ili kuikomboa Sudan yote, hadi Umm Dafuq. Minawi ameongeza kwamba hakuna mtu anayeweza kufuta alama za uhalifu uliofanywa na viongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, RSF.
Amekutaja hatua ya RSF ya kumkamata mmoja wa makamanda wake, Al-Fatih Idris, anayejulikana kama "Abu Lulu," na kumtuhumu kuwa amehusika na uhalifu dhidi ya raia huko Al-Fashir, kuwa ni mchezo wa kuigiza wa kisiasa ambao amesisitiza kwamba hautabadilisha ukweli.
Katika upande wa masuala ya kibinadamu, Madaktari Wasio na Mipaka wamethibitisha kwamba wakimbizi kutoka El Fasher wanawasili katika eneo la "Tawila" katika hali ya kusikitisha.
Tangu Vikosi vya Msaadai wa Haraka viudhibiti mji wa El Fasher, maelfu ya watu wamekimbilia eneo la Tawila huko Darfur Kaskazini (kilomita 60 kutoka El Fasher).
Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka imeongeza kuwa, zaidi ya watu 5,000 waliokimbia makazi yao wamewasili Tawila katika wiki moja tu, akieleza kuwa watoto wote waliofika wanasumbuliwa na utapiamlo, na zaidi ya 50% kati yao walikuwa katika hali mbaya.