Trump awakatia msaada ya chakula watu maskini nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133056-trump_awakatia_msaada_ya_chakula_watu_maskini_nchini_marekani
Huku mamilioni ya Wamarekani wakiendelea kupambana na ukosefu wa usalama wa chakula na uhaba wa chakula, utawala wa Trump umeamuru kukatwa kikamiifu msaada wa chakula kwa familia zenye kipato cha chini.
(last modified 2025-11-11T10:51:58+00:00 )
Nov 11, 2025 10:51 UTC
  • Trump awakatia msaada ya chakula watu maskini nchini Marekani

Huku mamilioni ya Wamarekani wakiendelea kupambana na ukosefu wa usalama wa chakula na uhaba wa chakula, utawala wa Trump umeamuru kukatwa kikamiifu msaada wa chakula kwa familia zenye kipato cha chini.

Wizara ya Kilimo ya Marekani imesema kwamba majimbo ya Marekani yatapunguziwa misaada kutoka Serikali ya Shirikisho ya majimbo hayo yataendelea kulipa marupurupu yao yote ya Msaada wa Chakula wa Nyongeza. Wizara hiyo imesisitiza kwamba malipo lazima yawe na kikomo chini ya amri ya Mahakama Kuu na majimbo ya Marekani lazima yabadilishe mara moja shughuli zao za huko nyuma.

Serikali ya Donald Trump imekuja kuvuruga Programu ya Msaada wa Chakula wa Nyongeza, ambayo inawanufaisha zaidi ya watu milioni 42 na hiyo ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 ya historia ya Marekani. Hayo ni katika hasara za kufungwa kwa muda mrefu shughuli za serikali Trump. Kufungwa huko kumeitia hasara Marekani ya zaidi ya dola bilioni 17 tangu Oktoba 1 na kumefanya maisha ya mamilioni wananchi kuwa magumu hasa hasa mamilioni ya familia zenye kipato cha chini huko Marekani.

Barua kutoka Wizara ya Kilimo ya Marekani imetoa vitisho ikisema kuwa jimbo lolote linalokaidi agizo hilo la Serikali ya Shirikisho litapoteza bajeti yake ya uendeshaji na litawajibika kwa malipo yoyote ya ziada. Wachambuzi wa mambo wameonya kwamba ikiwa mgogoro wa hivi sasa kisiasa na kifedha utaendelea, itakuwa tabu mno kwa mamilioni ya Wamarekani kupata angalau mlo mmoja kwa siku.