Utawala wa Kizayuni wakiri kupata hasara kubwa kufuatia mashambulizi ya Hizbullah
(last modified Wed, 04 Dec 2024 12:18:07 GMT )
Dec 04, 2024 12:18 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wakiri kupata hasara kubwa kufuatia mashambulizi ya Hizbullah

Mkuu wa kitongoji kimoja cha Wazayuni ameeleza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya nyumba ndani ya kitongoji hicho zimeharibiwa na kubomoka kufuatia mashambulizi ya makombora ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Akizungumzia hali ya sasa ya walowezi wa Kizayuni, David Azoulai, mkuu wa baraza la mji wa al-Mutla katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) amesema kuwa: "Tuko katika hali ngumu sana na hatujui iwaPO kuna chochote kilichosalia huko Matla au la."

Azoulai ameongeza kuwa: "Asilimia 75 nyumba katika eneo la Hartsafia zimemeharibiwa. Majengo mengi lazima yabomolewe kikamilifu kutokana na kuathiriwa pakubwa na mashambulizi ya makombora ya Hizbullah." 

Mashambulizi ya makombora ya Hizbullah ya Lebanon dhidi ya Wazayuni 

Kiongozi huyo wa Kizayuni ameashiria kuwa tayari yamewasilishwa maombi zaidi ya 20,000 ya kulipwa fidia na kusisitiza kuwa, uharibifu wa moja kwa moja wa mashambulizi hayo umesababisha hasara ya dola milioni 550 katika kitongoji hicho pekee.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel viliwahi kutangaza huko nyuma kuhusu hasara na maafa makubwa yaliyosababishwa na mashambulizi ya makombora ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.