Pars Today
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa watu 39 wameuawa shahidi na 123 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
Mtandao wa habari wa lugha ya Kiebrania wa Kan umedai kuwa Qatar imewaambia viongozi wa kisiasa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kwamba "hawatakiwi tena" katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
Kamati ya makundi ya mapambano na Muqawama ya Palestina imetoa taarifa kuhusu ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani na kutangaza kuwa, hakuna tofauti baina ya Warepublican na Wademokrat; Kwa sababu serikali zote za Marekani zimekuwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel na washirika wake katika mauaji dhidi ya taifa la Palestina.
Kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon kumeitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kimazingira na kiafya.
Mashabiki wa mpira wa Kizayuni waliokuwa wakitizama mechi ya soka katika mji wa Amsterdam nchini Uholanzi wameshambuliwa na kuchezea kipigo baada ya kuivunjia heshima bendera ya Palestina.
Hatua ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ya kumfuta kazi Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala huo imezidisha hali ya mgogoro huko Tel Aviv.
Miji mbalimbali ya Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu) hususan Tel Aviv iimeendelea kushuhudia maandamano makubwa ya kupinga hatua ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya kumfuta kazi Waziri wa Vita wa utawala huo, Yoav Gallant.
Kutokana na tangazo la kusitishwa shughuli za UNRWA, taasisi za kimataifa zimeonya kuhusu uwezekano wa kuzorota zaidi hali ya maisha ya Wapalestina hususan watoto, wanawake na wagonjwa huko Ukanda wa Gaza.
Wanamuqawama wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamevurumisha makombora katika kambi za kijeshi mahali walipokuwa wamekusanyika wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Bunge la Mpito la Mali limepitisha sheria inayojinaisha vitendo vya ufuska vya 'ushoga' na kujiunga na makumi ya nchi zingine za Kiafrika zilizopitisha sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo vinavyotetewa na Ulimwengu wa Magharibi kwa kisingizio cha haki za binadamu.