-
HRW: Saudia haiaminiki tena baada ya kudanganya kuhusu mauaji ya Khashoggi
Dec 07, 2018 14:30Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeutaka utawala wa Riyadh kuwaruhusu waangalizi huru kutathmini hali ya wanaharakati wanawake wanaozuiliwa katika jela za utawala huo wa kifalme, likisisitiza kuwa Saudi Arabia haiaminiki tena baada ya kutoa taarifa kadhaa za urongo kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi.
-
HRW: Askari usalama Msumbiji wanakiuka haki za binadamu
Dec 05, 2018 01:10Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limevituhumu vyombo vya usalama vya Msumbiji kuwa vinakiuka haki za binadamu katika operesheni zake za kupambana na ugaidi kaskazini mwa nchi.
-
HRW yaitaka Argentina ichunguze nafasi ya Bin Salman katika mauaji ya Khashoggi
Nov 27, 2018 07:51Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Argentina ifungue faili la kuchunguza nafasi ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman katika mauaji ya aliyekuwa mwandishi habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Aal-Saud, Jamal Khashoggi.
-
Amnesty: Saudia inawatesa wanaharakati kwa kuwabaka, kuwapiga kwa umeme
Nov 21, 2018 07:58Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limefichua kuwa, wapinzani na wanaharakati wa kisiasa nchini Saudi Arabia wanafanyiwa kila aina ya utesaji na udhalilishaji, ukiwemo udhalilishaji wa kingono, kupigwa kwa umeme na hata kupigwa mijeledi.
-
HRW: Misri inawazuilia kusikojulikana makumi ya watetezi wa haki za binadamu
Nov 18, 2018 14:27Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema vyombo vya usalama nchini Misri vimewatia nguvuni na kuwazuilia kusikojulikana makumi ya watetezi wa haki za binadamu tangu mwezi uliopita wa Oktoba hadi sasa.
-
Aal Saud na wimbi kubwa la ukosoaji na tahadhari za haki za binadamu
Nov 11, 2018 04:36Kufuatia kuuliwa Jamal Khashoggi mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal Saud katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul Uturuki na kufungwa jela huko Riyadh kundi kubwa la wapinzani wa jumuiya za kiraia, kisheria na kiaidiolojia; kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Saudia amekiri kuwa nchi hiyo imeonywa mara 258 na taasisi mbalimbali za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
-
Balozi: Wamagharibi wameipa Saudia kinga ya kufanya inachotaka
Oct 12, 2018 07:48Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London amesema utawala wa Aal-Saud umepewa kinga kamili na nchi za Magharibi ya kufanya unalotataka, na ndiposa hautaki hata kukosolewa juu ya mwenendo wake wa kueneza ugaidi na kukiuka haki za binadamu.
-
Utawala wa Aal Khalifa wavunja rekodi ya ukiukaji haki za binadamu nchini Bahrain
Oct 06, 2018 03:49Jumuiya ya haki za binadamu nchini Bahrain imetangaza kuwa katika mwezi mmoja tu wa Julai mwaka huu wa 2018, utawala wa Aal Khalifa umechukua hatua 844 za ukiukaji haki za binadamu dhidi ya raia wa nchi hiyo.
-
Amnesty yasajili jinai mpya za kivita nchini Sudan Kusini
Sep 19, 2018 07:26Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeituhumu serikali ya Sudan Kusini na makundi ya wabeba silaha yanayoungwa mkono na serikali hiyo kwamba yametenda jinai za kivita na ukatili wa kutisha dhidi ya raia.
-
Amnesty International yaitaka Saudia iwaachie huru watetezi wa haki za binadamu
Aug 08, 2018 04:13Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaka jamii ya kimataifa kuishinikiza zaidi Saudi Arabia ili ikomeshe ukandamizaji na iwaachie huru wapinzani na wanaharakati wa masuala ya kijamii. Wito huo umetolewa baada ya utawala wa kizazi cha Aal Saud kuzidisha mashinikizo dhidi ya wapinzani wa serikali ya kifalme ya nchi hiyo na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu.