Balozi: Wamagharibi wameipa Saudia kinga ya kufanya inachotaka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48742
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London amesema utawala wa Aal-Saud umepewa kinga kamili na nchi za Magharibi ya kufanya unalotataka, na ndiposa hautaki hata kukosolewa juu ya mwenendo wake wa kueneza ugaidi na kukiuka haki za binadamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 12, 2018 07:48 UTC
  • Balozi: Wamagharibi wameipa Saudia kinga ya kufanya inachotaka

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London amesema utawala wa Aal-Saud umepewa kinga kamili na nchi za Magharibi ya kufanya unalotataka, na ndiposa hautaki hata kukosolewa juu ya mwenendo wake wa kueneza ugaidi na kukiuka haki za binadamu.

Huku akiashiria habari ya kuuawa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudia huko mjini Istanbul, Uturuki, Hamid Baeidinejad amesema inashangaza namna wakosoaji wa utawala wa Riyadh wanavyouawa mchana kweupe tena nje ya nchi.

Balozi wa Iran mjini London amehoji, "Nchi za Magharibi zitaacha lini undumakuwili na haswa katika suala la ukiukaji wa haki za binadamu?"

Picha iliyobebwa na mwanaharakati ikiashiria mkono wa Bin Salman katika mauaji ya Khashoggi

Televisheni ya Uturuki imeonyesha mkanda wa video wa kuingia timu ya watu 15 kutoka Saudia, wakati wakitembea kutoka kwenye ndege binafsi kuelekea ulipo ubalozi mdogo wa utawala huo mjini Istanbul kwa ajili ya kufanya mauaji dhidi ya Jamal Khashoggi.

Gazeti la Washington Post linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa, Khashoggi aliuawa kwa amri ya Muhammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia