Iran yawasilisha ripoti rasmi UN kuhusu jinai za kivita za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128548-iran_yawasilisha_ripoti_rasmi_un_kuhusu_jinai_za_kivita_za_israel
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha ripoti rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na Israel wakati wa vita vyake vya siku 12 dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jul 20, 2025 09:35 UTC
  • Iran yawasilisha ripoti rasmi UN kuhusu jinai za kivita za Israel

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha ripoti rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na Israel wakati wa vita vyake vya siku 12 dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, mashtaka dhidi ya Israel, kwa ushahidi wa nyaraka za kina za mauaji ya raia na uharibifu wa miundombinu muhimu, yana umuhimu mkubwa kwa kambi ya Muqawama na takwa la kutambuliwa na kuheshimiwa uhuru na mamlaka ya kujitawala nchi.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasilisha faili hilo katika Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwaonyesha walimwengu kina cha jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni katika vita vya kutwishwa vya siku 12 dhidi ya taifa hili.

Kwa mujibu wa faili hilo lililowasilishwa na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, Tehran inataka Israel iwajibishwe na ibebeshwe dhima kupitia taasisi muhimu za kimataifa kama Umoja wa Mataifa.

Viongozi wa Iran wanasisitiza kuwa, mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni uhalifu wa kivita na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, na wameitaka jamii ya kimataifa ionyeshe radiamali.

Hata hivyo makamanda wa jeshi la Iran wanasema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haina imani na usitishaji vita uliopo, na kwamba imejiandaa kukabiliana na senario tofauti za uchokozi wa maadui.

Wameonya kwamba, kosa lolote litakalorudiwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litakabiliwa kwa jibu zito na kali zaidi, na ambalo litamfanya adui ajuitie uamuzi wake.