-
Mtandao wa wafungwa wa kisiasa Saudia wataka wanaharakati waachiwe huru kwa hofu ya corona
Mar 28, 2020 01:04Ukurasa wa mtandsao wa wafungwa wa kisiasa nchini Saudi Arabia umetoa wito wa watu kushiriki kwa wingi katika kampeni ya kuwaunga mkono wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari, maulamaa na wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa katika jela za Saudi Arabia.
-
HAMAS yasisitiza kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina nchini Saudi Arabia
Mar 23, 2020 08:14Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza juu ya ulazima wa kuachiliwa huru haraka iwezekanavyo wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Saudi Arabia
-
Bahrain yashinikizwa iwaachilie huru wafungwa wa kisiasa wanawake
Mar 09, 2020 11:28Jumuiya ya ‘Amani Kwa Ajili ya Demokrasia na Haki za Binadamu’ imewataka viongozi wa Bahrain kutambua haki za wanawake na hivyo kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa wanawake ambao wanashikiliwa kwa kosa kueleza mitazamo yao ya kisiasa au kuwa ni wanaharakati wa haki za binadamu.
-
Bahrain yamhukumu kifungo cha miaka 3 raia wa nchi hiyo aliyechoma moto bendera ya Israel
Feb 19, 2020 05:55Mahkama moja nchini Bahrain imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu raia wa nchi hiyo kwa kosa la kuchoma moto bendera ya utawala haramu wa Israel.
-
Uchunguzi: Al Sisi anawaua wapinzani wake kwa "mauti ya polepole" wakiwa jela
Feb 10, 2020 08:21Uchunguzi uliofanywa na televisheni ya al Jazeera ya Qatar umefichua takwimu za kutisha kuhusu idadi ya wafungwa wa kisiasa waliouawa au kuaga dunia kutokana na kutelekezwa, kutopatiwa matibabu kwa makusudi na mazingira mabaya kupita kiasi ndani ya jela za Misri tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na rais wa sasa wa nchi hiyo, Abdel Fattah al Sisi mwezi julai mwaka 2013.
-
Saudi Arabia yavunja rekodi yake ya kunyonga watu
Oct 07, 2019 07:55Katika kipindi cha miezi 9 iliyopita ya mwaka huu wa 2019, Saudi Arabia imeshatekeleza adhabu ya kifo kwa watu 160 na kuvunja rekodi yake ya huko nyuma ya kutekeleza adhabu hiyo kwa watu wengi zaidi duniani.
-
Baraza la kijeshi la uongozi wa mpito Sudan laahidi kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa
Jul 28, 2019 07:29Baraza la kijeshi la uongozi wa mpito la Sudan limetangaza kuwa limeamua kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa wenye mfungamno na Muungano wa Uhuru na Mabadiliko wa nchini humo.
-
Maandamano ya kupinga serikali yaendelea Bahrain, wanajeshi washambulia kinyama wafungwa
Apr 13, 2019 13:36Maandamano ya wananchi wa Bahrain ya kupinga utawala wa kiukoo na kupigania kuwa na utawala wa wananchi yanaendelea huku utawala wa kidikteta wa ukoo wa Aal Khalifa nao ukiendelea kukandamiza raia.
-
Wapinzani wanaozuiliwa Saudia waanza mgomo wa kula
Feb 19, 2019 15:45Shirika la kutetea haki za wafungwa la Prisoners of Conscience limetangaza kuwa, idadi kubwa ya wapinzani wanaozuiliwa katika jela za kuogofya za Saudi Arabia wameanza mgomo wa kula, kulalamikia hali ngumu na mateso wanayopitia wakiwa kizuizini.
-
Watoto 30 wanaoshikiliwa na utawala wa Bahrain wadhuriwa na chakula kilichoharibika
Oct 18, 2018 07:54Duru za habari nchini Bahrain zimeripoti kwamba utawala wa Aal-Khalifa umewapa chakula kilichoharibika watoto 30 unaowashikilia katika jela huku wasimamizi wake wakikataa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kuwapatia matibabu.