-
Pezeshkian: Maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na Tanzania ni fursa ya kipekee
Aug 01, 2024 06:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na baadhi ya maeneo ya Tanzania hasa Zanzibar, ni fursa nzuri ya kustawishwa zaidi na zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.
-
Rais Samia ataka ‘waliodumisha Muungano wa Tanzania waendelee kuenziwa'
Apr 26, 2024 14:31Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania waendelee kuwaenzi na kudumisha maono ya waasisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume pamoja na viongozi waliofuatia baada yao, kutokana na juhudi zao za kuujenga na kuudumisha Muungano huo.
-
Watalii wanne Waisraeli watimuliwa hotelini Zanzibar baada ya kulalamikia picha ya bendera ya Palestina
Apr 19, 2024 07:29Raia wanne wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamefukuzwa na kutolewa hotelini visiwani Zanzibar, Tanzania baada ya kulalamikia beji ya bendera ya Palestina iliyoandikwa juu yake maandishi ya kutetea uhuru wa Palestina.
-
Watu kadhaa wakamatwa kwa kula mchana wa Ramadhani Zanzibar
Mar 29, 2024 11:58Jeshi la polisi visiwani Zanzibar nchini Tanzania limewatia mbaroni watu 12 kwa tuhuma za kukiuka utaratibu wa dini ya Kiislamu kwa kula mchana hadharani katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Kampuni ya Ufaransa ya AGL yalalamikiwa kwa kutowajibika Bandarini Zanzibar + SAUTI
Dec 02, 2023 11:06Uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuikabidhi shughuli za uendeshaji wa Bandari ya Malindi kampuni ya Ufaransa ya AGL kwa lengo la kuongeza ufanisi katika bandari hiyo hauonekani kuzaa matunda yaliyokusudiwa kutokana na kampuni hiyo ya nchi ya Ulaya kulalamikiwa vikali.
-
Rais wa Zanzibar aadhimisha Siku ya Vyombo vya Habari kwa maagizo matano + SAUTI
May 04, 2023 02:10Jana Jumatano, Mei 3, 2023 ilikuwa ni siku ya vyombo vya habari. Rais Hussein Ali Hassan Mwinyi wa Zanzibari ametua fursa hiyo kutoa maagizo matano. Moja ya maagizo hayo ni kuwataka waandishi wa habari kutumia siku hiyo kuandaa hafla zinazohusu uhusiano kati ya uhuru wa vyombo vya habari, kujieleza na haki nyingine. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.
-
Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani lafanyika visiwani Zanzibar, Tanzania
Mar 19, 2023 12:39Kongamano la siku mbili la Idhaa za Kiswahili Duniani limeendelea leo visiwani Zanzibar nchini Tanzania kwa mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalamu wa lugha hiyo kutoka pembe tofauti za dunia.
-
Matukio ya Kiislamu wiki hii na Harith Subeit + Sauti
Mar 04, 2023 03:54Matukio ya Kiislamu wiki hii yamejumuisha maeneo tofauti ya Afrika Mashariki na Kati. Yameandaliwa na mwandishi wetu Harith Subeit. Ingia kwenye Sauti kusikiliza ripoti hiyo iliyo na matukio tofauti ya Kiislamu wiki hii.
-
Viongozi wa Tanzania watakiwa kutoa uhuru wa kisiasa + SAUTI
Nov 21, 2022 02:21Viongozi Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wametakiwa kuhakikisha harakati za kisiasa zinafanyika katika mazingira ya uhuru na haki nchini humo. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.
-
Nchi za Afrika zakutana Zanzibar kujadili maji safi na taka
Nov 15, 2022 07:51Nchi 42 za Afrika zinakutana Zanzibar nchini Tanzania kuanzia leo kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu udhibiti wa sekta ya maji safi na taka Afrika.