Apr 19, 2024 07:29 UTC
  • Watalii wanne Waisraeli watimuliwa hotelini Zanzibar baada ya kulalamikia picha ya bendera ya Palestina

Raia wanne wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamefukuzwa na kutolewa hotelini visiwani Zanzibar, Tanzania baada ya kulalamikia beji ya bendera ya Palestina iliyoandikwa juu yake maandishi ya kutetea uhuru wa Palestina.

Wazayuni hao wanne wametimuliwa katika hoteli ya kitalii ya Canary Nungwi Hotel huko Unguja kwenye visiwa vya Zanzibar baada ya kuanza kumsakama kwa masuali afisa mapokezi wa hoteli hiyoi juu ya gari iliyokuwa imeegeshwa kwenye eneo la hoteli ikiwa imebandikwa vipeperushi vinavyosomeka "Free Palestine", yaani "Palestina Huru".

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa MintPress, Waisraeli hao walifahamishwa kwamba gari lenye vipeperushi hivyo ni la meneja wa hoteli.

Pamoja na hayo, Wazayuni hao waliendelea kulalamikia suala hilo wakidai kwamba gari hilo linawafanya wawe na "wasiwasi" na ndipo uongozi wa hoteli ya Canary Nungwi ukachukua uamuzi wa kuwataka wafunge virago na kuhama hotelini humo.

Tangu utawala wa Kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari ya Wapalestina wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza Oktoba 7, 2023, -mauaji ambayo hadi sasa yameshasababisha Wapalestiina wanaokaribia 34,000 kuuawa shahidi wengi wao wakiwa wanawake na watoto-, wimbi la hisia za ghadhabu na chuki dhidi utawala huo limesambaa kila pembe ya dunia,sambamba na kuongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa uungaji mkono kwa taifa madhulumu la Palestina juu ya haki yao ya kuunda nchi yao huru katika maeneo yao yanayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Licha ya kampeni zinazofanywa na vyombo vya habari na madola ya Magharibii yakiongozwa na Marekani za kujaribu kuonyesha kuwa chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, zinaakisi chuki dhidii ya Mayahudi (Anti-Semitism), lakini mauaji ya kimbari ya Ghaza yameziamsha hisia na dhamiri za utu za walimwengu, bila kujali mbari, asili na dini zao, na kutangaza kuchukizwa kwao na utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.../

Tags