-
Miili 24 yatolewa kwenye migodi ya dhahabu nchini Zimbabwe
Feb 17, 2019 08:08Timu ya waokoaji imeopoa maiti 24 kwenye migodi ya dhahabu iliyoporomoka katika mji wa Kadoma, yapata kilomita 145 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
-
Rais wa Zimbabwe alaani ukandamizaji maandamano
Jan 22, 2019 14:52Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amelaani vikosi vyake vya usalama kwa kutumia mabavu kukandamiza maandamano ya wananchi waliokuwa wakilalamikia ughali ya maisha.
-
Wafanyakazi wa sekta ya umma Zimbabwe wakataa pendekezo jipya la nyongeza ya mishahara
Jan 19, 2019 15:33Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Zimbabwe wamekataa pendekezo la pili lililotolewa na serikali la nyongeza ya mishahara na kushikilia msimamo wao wa kutaka walipwe mishahara yao kwa kutumia sarafu ya dola ya Marekani.
-
Zimbabwe yatumia wanajeshi kuzima maandamano, kadhaa wauawa
Jan 15, 2019 14:38Watu wasiopungua watano wameuawa na maafisa usalama huku maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta kwa asilimia 150 nchini Zimbabwe yakishtadi.
-
Maandamano Zimbabwe baada ya ongezeko la bei ya mafuta kwa 150%
Jan 14, 2019 15:30Wananchi wa Zimbabwe hii leo wamefanya maandamano katika miji mikubwa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Harare, kulalamikia ongezeko la bei ya fueli kwa asilimia 150 lililotangazwa jana na Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo.
-
Miungano ya wafanyakazi Zimbabwe yakataa nyongeza ya asilimia 10 ya mshahara
Jan 11, 2019 15:58Watumishi wa umma nchini Zimbabwe kupitia miungano na vyama vya kutetea maslahi yao wamekataa nyongeza ya asilimia 10 ya mshahara iliyotangazwa na serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa jana Alkhamisi.
-
Walimu Zimbabwe kuanza mgomo Jumanne hii kuhusu mishahara yao
Jan 08, 2019 03:20Walimu nchini Zimbabwe wamesema kuwa leo Jumanne wanaanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara yao kwa sarafu ya dola ya Kimarekani. Hayo yameelezwa na muungano wa walimu wa nchi hiyo.
-
Polisi ya Afrika kusini yatoa waranti wa kukamatwa mke wa Mugabe
Dec 19, 2018 15:21Polisi ya Afrika Kusini imetoa kibali cha kutiwa nguvuni mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe kwa tuhuma za kumshambulia na kumpiga mwanamitindo Gabriella Engels mjini Johannesburg mwaka uliopita.
-
Hatimaye wapinzani wafanya maandamano nchini Zimbabwe
Nov 30, 2018 04:34Maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani wamefanya maandamano ya kupinga serikali mjini Harare Zimbabwe mbele ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo.
-
Serikali Zimbabwe yawaonya wapinzani wasithibutu kuandamana
Nov 27, 2018 14:49Serikali ya Zimbabwe imetoa onyo kwa chama cha upinzani cha MDC kuwa kitawajibika iwapo mpango wake wa maandamano yaliyopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii utasababisha vifo, majeruhi au uharibifu wa mali.