-
Maveterani Zimbabwe: Jeshi kama lingechelewa kumtimua Mugabe, tungemtimua sisi
Dec 29, 2017 12:33Mashujaa wa vita vya ukombozi nchini Zimbabwe wametangaza kwamba, walikuwa wamepanga mkakati wa kumuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe wiki chache kabla ya jeshi kumtimua.
-
Mkuu wa zamani wa vikosi vya ulinzi Zimbabwe aapishwa; Mugabe nae apatiwa haki za kidiplomasia
Dec 29, 2017 00:11Mkuu wa vikosi vya ulinzi wa Zimbabwe aliyejiuzulu ambaye aliongoza mapinduzi yasiyo ya umwagaji damu na kuhitimisha utawala wa miaka 37 wa Robert Mugabe jana Alhamisi aliapishwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo na hivyo kuwa kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi kuingia serikalini.
-
Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe aliyejiuzulu kuapishwa kuwa makamu wa rais
Dec 28, 2017 04:28Aliyekuwa Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi nchini Zimbabwe Jenerali Constantino Chiwenga ambaye aliongoza mapinduzi baridi ya kijeshi dhidi ya Robert Mugabe anatazamiwa kuapishwa leo Alkhamisi kuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo.
-
Mnangagwa amteua aliyekuwa mkuu wa jeshi Zimbabwe kuwa naibu wake
Dec 24, 2017 04:38Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amemteua Kamanda wa Vikosi vya Ulinzi aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita, Jenerali Constantino Chiwenga kuwa naibu wake ndani ya chama tawala Zanu-PF.
-
Rais wa Zimbabwe: Lazima chama tawala kirekebishe uchumi ili kuweza kushinda uchaguzi ujao
Dec 16, 2017 04:40Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewaeleza wanachama wa chama chake tawala cha ZANU-PF kuwa wanapaswa kuurekebisha uchumi ikiwa wanataka wawe na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
-
Rais wa Zimbabwe ameazimia kupambana na ufisadi
Dec 15, 2017 04:12Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameazimia kupambana na ufisadi na kusema atawataja na kuwaaibisha wote waliopeleka fedha za umma nje ya nchi kama watashindwa kuzirudisha.
-
Mabadiliko ya kisiasa Zimbabwe baada ya Mugabe na mustakabali unaoikabili nchi hiyo
Dec 03, 2017 09:43Baada ya kupita wiki chache tangu kuingia madarakani rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na kutangaza baraza lake jipya la mawaziri, malalamiko dhidi ya uteuzi aliofanya yamemfanya alazimike kuwabadilisha mawaziri wake wawili baada ya kupita siku mbili tu tangu alipowateua.
-
Mawaziri wawili wafutwa kazi siku mbili tu tangu wateuliwe nchini Zimbabwe
Dec 02, 2017 23:34Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana aliwafuta kazi mawaziri wake wawili zikiwa zimepita siku mbili tu tangu awateuwe siku ya Alkhamisi.
-
Mnangagwa ateua baraza la mawaziri, wanajeshi na wapambe wa Zanu-PF wafaidi
Dec 01, 2017 04:06Emmerson Mnangagwa, Rais mpya wa Zimbabwe ameteuwa baraza lake jipya la mawaziri, linalojumuisha maafisa wa ngazi za juu kwenye jeshi la nchi hiyo na viongozi 'waaminifu' wa chama tawala ZANU-PF.
-
Rais Mnangagwa wa Zimbabwe atoa muhula wa miezi mitatu kwa walioiba fedha za umma kuzirejesha
Nov 29, 2017 00:55Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametoa muhula wa miezi mitatu kwa wale wote waliopora fedha za umma na kuzificha nje ya nchi kuzirejesha.