-
Wauguzi Zimbabwe wamaliza mgomo wao wa miezi mitatu
Sep 09, 2020 07:15Chama kikuu cha wauguzi nchini Zimbabwe kimetangaza leo Jumatano kwamba kinawahamasisha wanachama wake kumaliza mgomo wao wa kulalamikia mishahara yao ambao ulianza mwezi Juni mwaka huu. Mgomo huo wa miezi mitatu umezilazimisha hospitali kuu za nchi hiyo kushindwa kupokea wagonjwa tena wakati huu wa janga la COVID-19.
-
Zimbabwe: Wakulima wazungu wa kigeni wanaweza kuwasilisha maombi ili kurejeshewa ardhi zao walizonyang'anywa
Sep 01, 2020 08:12Wakulima wazungu waliohamia Zimbabwe ambao walinyang'anywa ardhi zao za kilimo wakati wa utawala wa Rais Robert Mugabe wanaweza kuwasilisha maombi ili kurejeshewa ardhi hizo.
-
Zimbabwe kuwalipa wakulima wazungu fidia ya dola bilioni 3.5
Jul 30, 2020 06:07Serikali ya Zimbabwe imeafiki kuwalipa wakulima wazungu fidia ya dola bilioni 3.5 kutokana na ardhi zao kuchukuliwa na serikali kwa ajili ya kuwapa wenyeji Waafrika.
-
Rais wa Zimbabwe awashambulia Wamagharibi kwa kuingilia masuala ya ndani ya Afrika
May 25, 2020 21:57Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amezishambulia vikali nchi za Magharibi kwa kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya mataifa ya Afrika.
-
Chama kikuu cha upinzani Zimbabwe chaitaka polisi ieleze waliko wanaharakati waliotoweka
May 15, 2020 03:24Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Harakati kwa ajili ya Mabadiliko ya Kidemokrasia (MDC) kimesema, wanaharakati wake watatu wametoweka baada ya kushiriki maandamano ya kulalamikia uhaba wa chakula; na polisi inakana kuwashikilia wakati awali ilivieleza vyombo vya habari vya ndani kwamba wanaharakati hao walikuwa wamekamatwa.
-
Alkhamisi, tarehe 7 Mei, 2020
May 07, 2020 21:01Leo ni tarehe 13 Ramadhani 1441 Hijria sawa na Mei 7 mwaka 2020.
-
Uganda yashtakiwa EACJ kwa 'sheria kandamizi' za kudhibiti corona
Apr 11, 2020 06:41Wakili mmoja wa Uganda ameishtaki serikali ya Rais Yoweri Museveni katika Mahakama ya Uadilifu ya Afrika Mashariki EACJ akitaka kuondolewa zuio la kutoka nje lililotangazwa na serikali kama moja ya njia za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 (corona) nchini humo.
-
Afrika Kusini kujenga uzio katika mpaka wake na Zimbabwe
Mar 20, 2020 09:57Serikali ya Afrika Kusini imesema inajiandaa kujenga uzio wa kilomita 40 katika mpaka wa nchi hiyo na Zimbabwe, kwa lengo la kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini humo, na pia kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Corona nchini humo.
-
Hofu yatanda baada ya mshukiwa wa Corona kutoroka karantini Zimbabwe
Mar 10, 2020 04:48Hali ya taharuki imetanda nchini Zimbabwe baada ya mtu anayeshukiwa kuwa na virusi vya Corona kutoroka hospitalini alikokuwa amewekwa karantini na kwenda kusikojulikana.
-
WFP: Zimbabwe inakabiliwa na hatari ya baa kubwa la njaa
Dec 31, 2019 09:30Zimbabwe inakabiliwa na hatari ya baa kubwa la njaa ambapo karibu watu milioni 8 sawa na nusu ya watu wote wa nchi hiyo hawana uhakika wa chakula.