-
UN yasema kunyimwa dhamana Besigye na mahakama ya Uganda kunatia hofu kubwa
Aug 14, 2025 09:36Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema mwenendo wa Mahakama Kuu ya Uganda wa kumnyima dhamana mara kwa mara kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo Kizza Besigye pamoja na msaidizi wake Obeid Lutale katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa.
-
Watu 25 wafukiwa na kifusi Tanzania wakati shughuli za ukarabati mgodi
Aug 14, 2025 03:23Watu 25 wamefukiwa na kifusi katika mgodi mdogo wa dhahabu unaomilikiwa na Kikundi cha Wachapakazi, uliopo Kijiji cha Mwongozo, Kata ya Mwenge, Halmashauri ya Shinyanga, mkoani Shinyanga nchini Tanzania, baada ya mgodi huo kutitia wakati wa zoezi la ukarabati wa maduara.
-
Sudan Kusini yakanusha kukubali kuwapokea Wapalestina kutoka Gaza
Aug 14, 2025 03:10Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan Kusini imekanusha ripoti zinazosema kwamba imefanya mazungumzo na Israel kuhusu suala la kuwapokea Wapalestina kutoka eneo la Gaza lililokumbwa na vita.
-
Uhamiaji wa kulazimishwa dhidi ya Wapalestina wa Gaza; kwa nini Israel inaitazama Afrika?
Aug 14, 2025 01:03Katika hali ambayo vita vya Gaza vinaendelea na hali mbaya ya kibinadamu katika ukanda huo imefikia kiasi kwamba makumi ya wakazi wa Gaza wanakufa kila siku, si tu kwa kupigwa risasi na askari wa Israel bali pia kutokana na njaa na kiu kali, Israel inafanya mazungumzo na nchi kadhaa za Kiafrika ili kuwahamishia huko kwa nguvu wakazi wa Gaza.
-
Je Sudan Kusini ndio kituo kipya cha mpango wa kuwahamisha Wagaza kwa lazima?
Aug 14, 2025 00:09Chombo kimoja cha habari cha lugha ya Kiebrania kimetangaza kuwa, huku mashambulizi na vita katika Ukanda wa Gaza vikiendelea, Israel inafanya mazungumzo na Sudan Kusini, Indonesia, Libya, Ethiopia na nchi nyingine kadhaa za Kiafrika ili kuwapokea wakaazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Al-Burhan asisitiza kutoshirikishwa RSF katika mustakabali wa Sudan
Aug 13, 2025 07:30Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan, amesisitiza kuwa, Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) hakitakuwa na nafasi katika mustakabali wa nchi hiyo.
-
Al-Sisi: Misri haitafumbia macho haki yake ya maji
Aug 13, 2025 03:46Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, amesema kwamba mtu yeyote anayedhani kwamba Misri itafumbia macho haki yake ya kunufaika na maji ya Mto Nile anakosea.
-
Mapigano makali yaibuka tena kati ya jeshi la Kongo na M23
Aug 12, 2025 23:00Mapigano makali yameibuka baina ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Kundi la waasi wa M23, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi uliopita wa Julai.
-
RSF yashambulia kambi ya Abu Shouk Darfur Kaskazini
Aug 12, 2025 22:59Wanamgambo wa RSF wameishambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk katika mkoa wa Darfur Kaskazini na kusababisha mauaji ya watu 40 huku wengine 19 wakijeruhiwa vibaya.
-
Rwanda yalaani ripoti ya Umoja wa Mataifa kwamba ilisaidia waasi wa M23 kuua raia
Aug 12, 2025 09:30Serikali ya Rwanda imelaani ripoti ya umoja wa Mataifa ya wiki iliyopoita, kuwa jeshi lake lililisaidia kundi la waasi wa M23 kuwauwa mamia ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.