-
Amnesty yaikosoa Nigeria kwa kuwakandamiza Waislamu wakiitetea Gaza
Aug 21, 2025 01:43Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International nchini Nigeria, Isa Sunusi, amelaani vikali ukandamizaji mkali wa vyombo vya serikali dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, wakati wa maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kusema kuwa takriban wanachama 83 wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria bado wako rumande bila kufunguliwa mashtaka, licha ya kupata majeraha ya risasi na makovu mengineo wakishiriki maandamano ya amani.
-
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan: Tunafanya kazi kwa bidii kudhibiti usalama na uwepo wa kigeni nchini
Aug 21, 2025 08:14Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan, Luteni Jenerali Babiker Samra amesema kwamba uwepo haramu wa wapiganaji wa kigeni nchini humo hauwezi tena kuvumiliwa, kutokana na athari zake mbaya za kiusalama, kiuchumi na kijamii.
-
Ajali ya boti yaua watu wasiopungua 22 kaskazini magharibi mwa Nigeria
Aug 20, 2025 23:52Watu wasiopungua 22 wanaaminika kuwa wameaga dunia baada ya boti waliyokuwa wameabiri ndani yake kuzama kaskazini magharibi mwa Nigeria. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la huduma za dharura la nchi hiyo.
-
Katibu Mkuu wa UN: Afrika inapasa iwe ya kwanza kunufaika na madini yake muhimu
Aug 20, 2025 23:32Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na Afrika, akisisitiza kwamba nchi zinazoshikilia utajiri mkubwa wa madini wa bara hilo lazima ziwe za kwanza kunufaika.
-
Kwa nini utawala wa kizayuni wa Israel unataka kuzidisha satua na ushawishi wake barani Afrika?
Aug 20, 2025 23:29Katika mwendelezo wa hatua za kujaribu kuwa na satua na ushawishi katika nchi za Kiafrika, waziri wa mambo ya nje wa utawala wa kizayuni wa Israel Gideon Saar siku ya Jumanne alielekea Zambia katika safari ya kidiplomasia barani Afrika, madhumuni makuu yakiwa ni kufungua ubalozi wa utawala huo haramu nchini humo.
-
HRW: Waasi wa M23 wameuwa raia zaidi ya 140 mashariki mwa Kongo
Aug 20, 2025 08:28Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeeleza hii leo kuwa waasi wa kundi la M23 limeuwa raia zaidi ya 140 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje: Uganda haijakubaliana na Marekani kupokea wahamiaji haramu
Aug 20, 2025 08:27Uganda imesema kuwa haijafikia makubaliano na Marekani kuwapokea nchini humo wahamiaji haramu kwa sababu haina miundomsingi inayohitajika kufanya hivyo.
-
Watu 27 wauawa katika shambulio la kigaidi msikitini Nigeria
Aug 20, 2025 03:16Magaidi waliokuwa na silaha jana Jumanne waliwauwa waumini karibu 27 waliokuwa msikitini katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Sudan yaripoti wagonjwa wapya wa kipindupindu 1,575, vifo 22
Aug 20, 2025 03:00Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kuwa wagonjwa 1,575 wapya wa kipindupindu na vifo 22 vimesajiliwa kote nchini humo katika muda wa wiki moja iliyopita.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchaguzi mkuu Disemba 28
Aug 20, 2025 02:57Jamhuri ya Afrika ya Kati itaendesha uchaguzi mkuu Disemba 28 mwaka huu baada ya kuakhrishwa mara kadhaa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya jana Jumanne.