-
Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim aaga dunia, amezikwa leo
Jul 10, 2025 09:43Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim Hussein Athman amefariki dunia usiku wa manane wa kuamkia leo mjini Mombasa na maziko yake yamefanyika leo.
-
Mahakama Kenya yaiamuru polisi iache kufunga jiji la Nairobi wakati wa maandamano
Jul 10, 2025 03:34Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa amri ya kuwazuia polisi kuweka vizuizi au kuzuia raia kufika katikati mwa jiji la Nairobi wakati wa maandamano. Jaji wa mahakama hiyo Lawrence Mugambi alitoa amri hiyo jana Jumatano kufuatia kesi iliyowasilishwa na Katiba Institute baada ya jiji kufungwa wakati wa maandamano ya Saba Saba mnamo Jumatatu wiki hii.
-
Wawakilishi wa Serikali ya DRC na M23 wawasili Qatar kwa mazungumzo
Jul 10, 2025 02:43Wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 wamewasili katika mji mkuu wa Qatar, Doha kwa mazungumzo mapana kuhusu makubaliano. Hayo yameelezwa na mwanadiplomasia mmoja anayefahamu yanayojiri kuhusu mazungumzo hayo.
-
Rais wa Kenya aonya kuhusu njama ya kupindua serikali kupitia maandamano
Jul 09, 2025 10:52Rais wa Kenya William Ruto siku ya Jumatano aliwashutumu wapinzani wake wa kisiasa kwa kupanga njama ya kupindua serikali yake, akionya kuwa mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi na maandamano yenye vurugu yatatafsiriwa kama vitendo vya kivita.
-
Waendesha mashtaka Kenya: Waandamanaji 37 watafunguliwa mashtaka ya ugaidi
Jul 09, 2025 04:35Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itafungua mashtaka ya ugaidi dhidi ya watu 37 waliokamatwa kwenye maandamano ya kuipinga serikali mwishoni mwa mwezi Juni.
-
Rais wa Sudan Kusini amuuzulu mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu kwa miezi 7 tu
Jul 09, 2025 04:24Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miezi saba tu na kumtangaza mkuu mpya atakayeshika nafasi hiyo.
-
Asasi: Waasi, majambazi Nigeria wameua zaidi katika nusu ya kwanza ya 2025 kuliko 2024
Jul 08, 2025 11:04Idadi ya watu waliouawa na majambazi au waasi nchini Nigeria katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ni kubwa mno kuliko idadi ya waliouawa mwaka wote wa 2024, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana Jumanne na shirika la haki za binadamu la Nigeria.
-
Umoja wa Mataifa 'washtushwa' na mauaji ya waandamanaji Kenya
Jul 08, 2025 10:50Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya vifo vya watu zaidi ya 10 nchini Kenya, ambapo polisi na waandamanaji walikabiliana wakati wa maandamano ya kupinga sera za serikali ya nchi hiyo Jumatatu.
-
Rais wa Afrika Kusini ajibu bwabwaja na vitisho vya Trump
Jul 08, 2025 10:09Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amejibu matamshi ya vitisho na ubabe ya Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye hivi karibuni alitishia kuongeza ushuru wa asilimia kwa nchi ambazo zinajiegemeza na kufungamana na "sera za kupambana na Marekani" za jumuiya ya kiuchumi ya BRICS.
-
Nembo ya ‘Made in Tanzania' yazinduliwa katika Maonesho ya Sabasaba 2025
Jul 08, 2025 09:09Tanzania imezindua rasmi nembo ya ‘Made in Tanzania’ kwa lengo la kutangaza bidhaa zinazotengenezwa nyumbani kimataifa na kuitangaza Tanzania kama nchi ambayo inatengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, ubunifu na hasa zenye asili ya Kiafrika.