-
Wanajeshi wa Afrika Kusini waanza kuondoka DRC
May 04, 2025 08:06Afrika Kusini imeanza mchakato wa kuondoa wanajeshi wake wa kulinda amani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kikosi cha kwanza kimeondoka mapema wiki hii.
-
RSF yafanya shambulio la kwanza la droni Port Sudan
May 04, 2025 04:13Msemaji wa jeshi la Sudan ametangaza leo kuwa wanamgambo wa kikosi cha RSF wamefanya shambulio la ndege isiyo na rubani (droni) katika kambi ya jeshi la nchi hiyo na katika vituo vingine karibu na uwanja wa ndege wa Port Sudan. Hili ni shambulio la kwanza kuwahi kufanywa na wanamgambo wa RSF katika mji huo wa bandari wa mashariki.
-
Misri: Haiwezekani kupuuza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Israel
May 04, 2025 04:12Mwakilishi wa Misri katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) amesema: "Katika muda mrefu, haiwezekani kupuuza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, kama chombo kikuu cha mahakama cha Umoja wa Mataifa."
-
Waasi wa RSF wameua raia 300 huko Al-Nahud
May 03, 2025 23:01Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Sudan imetangaza kwamba raia wasiopungua 300, wakiwemo watoto 21 na wanawake 15, wameuawa katika shambulio lililofanywa na waasi wa RSF katika mji wa Al-Nahud, jimbo la Kordofan Magharibi.
-
Watu 27 wauwawa baada RSF kuteka mji muhimu Sudan
May 03, 2025 07:39Watu wasiopungua 27 wameuawa baada ya kundi la wapiganaji wa vikosi vya RSF, linaloongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kuripotiwa kuwa limefanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa En Nahud nchini Sudan.
-
Katika tukio la magendo ya binadamu, Polisi Afrika Kusini yaokoa Waethiopia 44 wakiwemo watoto 17
May 03, 2025 03:26Polisi ya Afrika Kusini imetangaza kuwa imewaokoa raia 44 wa Ethiopia ambao wanadaiwa kuzuiliwa katika eneo tajiri la jiji la Johannesburg.
-
UN inahitaji msaada wa dharura wa kuwasaidia wahanga 45,000 wa mafuriko Somalia
May 02, 2025 22:49Shirika moja la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu limesema kuwa linahitaji msaada wa dharura wa haraka wa kusaidia watu 45,000 walioathiriwa na mafuriko kote nchini Somalia.
-
Namibia imerekodi zaidi ya kesi 56,000 za malaria tangu Disemba
May 02, 2025 22:48Waziri wa Afya wa Namibia, Esperance Luvindao amesema kuwa nchi yake imerekodi kesi 56,130 za malaria na vifo 95 tangu ulipoanza msimu wa hivi sasa wa maambukizi makubwa ya malaria yaani mwezi Disemba 2024,
-
Wanawake wa Morocco wadai usawa katika kazi za nyumbani, wataka wanaume nao wavae "aproni" za jikoni
May 02, 2025 03:45Kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, makumi ya wanawake wa Morocco wamefanya maandamano kwenye mitaa ya Casablanca wakisisitiza umuhimu wa kazi za nyumbani zisizo na malipo na kudai usawa wa kijinsia katika kugawana kazi za nyumbani.
-
UN: Ukatili unaofanyika Sudan hauna mipaka; vifo vyaongezeka Darfur
May 01, 2025 23:23Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 540 wameuawa huko Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan katika muda wa wiki tatu zilizopita, huku wanajeshi wakizidisha opereseheni zao za kuukomboa mji wa el-Fasher, makao makuu ya jimbo hilo.