-
Pandor ahimiza mageuzi ya kimataifa kutekeleza uamuzi wa ICJ kuhusu Gaza
Apr 22, 2025 22:42Naledi Pandor Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa kushindwa kusitishwa mashambulizi na mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza kumefichua mapungufu ya mifumo ya kisheria ya kimataifa na kuibua upya wito kuhusu udharura wa kufanyika mageuzi katika Umoja wa Mataifa.
-
WFP: Matibabu ya utapiamlo yasitishwa nchini Ethiopia kutokana na ukosefu wa fedha
Apr 22, 2025 22:39Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wiki hii umesimamisha matibabu ya utapiamlo kwa wanawake na watoto 650,000 nchini Ethiopia kutokana na uhaba mkubwa wa fedha. WFP imesema kuwa mamilioni ya watu wako katika hatari ya kukosa misaada.
-
Maandamano ya wananchi Morocco; nara dhidi ya jinai za Israel
Apr 22, 2025 09:41Wananchi wa Morocco wameandamana kuunga mkono Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza na kupinga meli zinazobeba zana za kijeshi za utawala wa Kizayuni kutia nanga katika bandari za nchi yao.
-
Jeshi la Sudan Kusini: Tumeukomboa mji muhimu kutoka mikononi mwa Jeshi Jeupe
Apr 22, 2025 05:16Jeshi la Sudan Kusini limetangaza kuwa limeukomboa mji muhimu katika jimbo la Upper Nile ambao ulikuwa umetekwa na wanamgambo wa kabila la Nuer mwezi Machi katika mapigano ambayo yalipelekea kuwekwa kwenye kizuizi cha nyumbani Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar na kuibua mzozo mkubwa wa kisiasa nchini humo.
-
Serikali ya CAR yatangaza mazungumzo na upinzani miezi michache kabla ya uchaguzi wa urais
Apr 21, 2025 23:27Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa, inataka kufanya mazungumzo ya kisiasa na mrengo wa upinzani ikiwa ni miezi michache kabla ya uchaguzi wa urais mwezi Desemba mwaka huu.
-
Rais wa Kenya aelekea China baada ya Marekani kuongeza ushuru
Apr 21, 2025 07:16Ziara ya siku tano ya Rais wa Kenya William Ruto nchini China inayoanza Jumanne imetajwa kuwa hatua muhimu katika mwelekeo wa kidiplomasia na kiuchumi wa Kenya, huku akilenga kukabiliana na hatua mpya zilizochukuliwa dhidi ya nchi hiyo na Marekani.
-
UN: Operesheni za misaada na mapigano Kaskazini mwa Darfur, Sudan
Apr 21, 2025 07:06Mashirika ya misaada yanakumbana na matatizo makubwa katika kukabiliana janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya Kaskazini mwa Darfur, Sudan, linalosababishwa na mashambulizi ya waasi wa kundi la Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Papa wa Misri: Wapalestina wa Gaza wanakabiliwa na dhulma za kuogofya
Apr 20, 2025 22:56Papa Tawadros II, Kiongozi wa Kanisa la Kiorthodoksi la Coptic la Misri, amelaani vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kuyataja kama "moja ya aina mbaya zaidi za dhuluma" dhidi ya Wapalestina.
-
Wanajeshi 70 wa Benin wauawa katika shambulio la kigaidi
Apr 20, 2025 09:26Kundi la kigaidi la Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda limetangaza kuwa wapiganaji wake wameua wanajeshi 70 katika mashambulizi dhidi ya vituo viwili vya kijeshi kaskazini mwa Benin.
-
Shughuli za chama cha Kabila zasitishwa na serikali ya DRC
Apr 20, 2025 08:44Mali za rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila zimevamiwa na vyombo vya usalama na shughuli za chama chake zimesimamishwa nchi nzima.