-
UNICEF: Watoto Sudan wanakabiliwa na machungu yasiyoelezeka
Mar 14, 2025 03:20Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema vita vinavyoendelea Sudan ni janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani, likiwaacha watoto katika hali mbaya zaidi.
-
Tanzania yatangaza kumalizika mlipuko wa Marburg
Mar 13, 2025 22:59Tanzania jana Alkhamisi ilitangaza mwisho wa mlipuko wa virusi vya Marburg, kwani hakuna kesi yoyote mpya iliyoripotiwa nchini humo katika kipindi cha siku 42.
-
UNHCR: Ghasia Sudan Kusini zimelazimisha watu 10,000 kukimbilia Ethiopia
Mar 13, 2025 22:59Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema ghasia katika kaunti za kaskazini mwa Sudan za Nasir na Ulang zimeongezeka kwa kasi, na kuwalazimu zaidi ya watu 10,000 kukimbilia nchi jirani ya Ethiopia.
-
Sasa mazungumzo baina ya serikali ya DRC na waasi wa M23 kufanyika Jumanne ijayo
Mar 13, 2025 06:27Tarehe ya mazungumzo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na waasi wa M23 imetangazwa. Sasa pande hizo mbili zitafanya mazungumzo ya ana kwa ana ya amani Jumanne ijayo ya Machi 18, 2025 huko Luanda, mji mkuu wa Angola.
-
IGAD yatakiwa kuishawishi Sudan Kusini kuwachilia huru wapinzani
Mar 13, 2025 06:27Chama kikuu cha upinzani huko Sudan Kusini, cha Sudan People's Liberation Movement/Army-In Opposition (SPLM/A-IO) kinachoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Riek Machar, kimezihimiza Jumuiya ya IGAD na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kuingilia kati na kusaidia kuachiliwa huru maafisa kadhaa wa upinzani wanaoshikiliwa na serikai ya Sudan Kusini.
-
Jeshi: Watu 10 wauawa, 23 wajeruhiwa katika shambulio la RSF Sudan
Mar 13, 2025 06:25Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kuwa, takriban watu 10 wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye vitongoji vya makazi ya watu huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini la magharibi mwa Sudan.
-
UN: Zaidi ya watu milioni 30 nchini Sudan wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu
Mar 13, 2025 04:13Zaidi ya watu milioni 30 katika nchi iliyoathiriwa na vita ya Sudan wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu huku hali ya maisha ikizidi kuwa mbaya. Haya yalielezwa jana Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
-
Nigeria yathibitisha vifo vipya vitano kutokana na homa ya Lassa
Mar 12, 2025 22:51Nigeria imethibitisha vifo vipya vitano kutokana na homa ya Lassa, ugonjwa ambao umesambaa katika eneo la magharibi mwa Afrika.
-
Kongo yashindwa kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Mpox
Mar 12, 2025 22:51Wiki sita baada ya waasi wanaoungwa mkono na Rwanda kuteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, eneo hilo linakabiliwa na hali mbaya katika mapambano yake dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa mpox.
-
ANC: Afrika Kusini haitakubali Kutishwa na Marekani
Mar 12, 2025 09:10Naibu Katibu Mkuu wa kwanza wa chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, Nomvula Mokonyane, amekemea wanachama wa chama cha Democratic Alliance (DA) ambao wamekwenda Marekani kujipendekeza kwa rais wan chi hiyo Donald Trump na kutaja hatua hiyo kama dharau kwa uhuru wa nchi hiyo.