-
Rwanda: Serikali ya Uingereza imevunja uaminifu
Mar 04, 2025 08:16Serikali ya Rwanda imeishutumu Uingereza kwa kile ilichokita kuwa kuvunja uaminifu na kuchukua hatua zisizo na msingi dhidi ya Kigali, na imeitaka serikali ya Uingereza iilipe Rwanda kiasi cha pauni milioni 50 chini ya mpango wa Ushirikiano wa Wahamiaji na Maendeleo ya Kiuchumi ambao haupo kwa sasa.
-
Wabunge wa Ghana wawasilisha mswada wa kuongeza adhabu kwa wapenzi wa watu wa jinsia moja
Mar 04, 2025 07:55Wabunge wa Ghana wamewasilisha tena mswada dhidi ya mahuusiano ya kiimapenzii ya watu wa jinsia moja (LGBTQ), baada ya jaribio la awali kushindikana kwa sababu ya changamoto za kisheria.
-
Umoja wa Mataifa: Watoto wa mwaka mmoja ni miongoni mwa waliobakwa Sudan
Mar 04, 2025 07:44Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watu wenye silaha wanabaka na kuwanyanyasa kingono watoto wenye umri hadi mwaka mmoja katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.
-
Kenya nayo yajiandaa kukabiliana na ugonjwa usiojulikana
Mar 03, 2025 23:29Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza kuwa, imo mbioni kupambana na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana ambao umeathiri zaidi ya watu 200 katika vijiji vitatu vya jimbo la Kisii eneo la Nyanza Magharibi ya nchi hiyo.
-
Rwanda: Aliyekuwa mkuu wa Kitivo cha Tiba cha Butare ashtakiwa Paris kwa Mauaji ya Kimbari
Mar 03, 2025 23:29Mkuu wa zamani wa Kitivo cha Tiba cha Butare nchini Rwanda ameshtakiwa mjini Paris Ufaransa kwa mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na kula njama ya kutenda uhalifu.
-
Kenya inazungumza na Thailand juu ya kuwarejesha raia 64 waliokwama Myanmar
Mar 03, 2025 10:57Kenya inafanya mazungumzo na Serikali ya Thailand ili kufungua tena mpaka wa nchi hiyo na Myanmar, ikitaka kuwahamisha raia 64 wa Kenya waliookolewa hivi karibuni kutoka kwenye mitandao ya magendo ya binadamu nchini Myanmar.
-
Jordan yapinga juhudi za RSF za kuunda serikali nyingine nchini Sudan
Mar 03, 2025 10:16Jordan imepinga juhudi zozote zinazoweza kuhatarisha umoja wa Sudan, ikiwa ni pamoja na jitihada za kuundwa serikali nyingine ambazo zinafanywa na wapinzani wa jeshi la Sudan na imesema kuwa jambo hilo linaweza kushadidisha tu mgogoro wa Sudan.
-
Rais wa Guinea-Bissau atishia kuufukuza ujumbe wa ECOWAS
Mar 03, 2025 03:37Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo ametishia kuufukuza ujumbe wa kisiasa uliotumwa nchini mwake na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
-
Uganda yatuma wanajeshi zaidi DRC, huku mzozo ukiendelea
Mar 02, 2025 22:54Jeshi la Uganda limethibitisha kutuma wanajeshi wake katika mji mwingine kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupambana na makundi yenye silaha, huku kukiwa na hofu kuwa mzozo mkali unaoendelea DRC unaweza kuingia katika vita vikubwa.
-
Wanajeshi 11 wauliwa kaskazini mwa Niger
Mar 02, 2025 22:53Wanajeshi wasiopungua 11 wameuawa kaskazini mwa Niger na wengine kadhaa wamejeruhiwa.