-
Wanajeshi 11 wauliwa kaskazini mwa Niger
Mar 02, 2025 22:53Wanajeshi wasiopungua 11 wameuawa kaskazini mwa Niger na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
-
WHO: Uganda imeripoti kifo kingine cha Ebola
Mar 02, 2025 08:56Shirika la Afya Duniani WHO likinukuu Wizara ya Afya ya Uganda limesema mgonjwa wa pili wa Ebola amefariki dunia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Misri yapinga kuundwa serikali nyingine nchini Sudan
Mar 02, 2025 08:54Misri imetangaza leo Jumapili kuwa haiafiki jaribio lolote la kuunda serikali nyingine nchini Sudan au kuchukuliwa hatua yoyote ambayo inatishia umoja na mamlaka ya kujitawala Sudan.
-
Mapigano mashariki mwa DRC yazidisha mateso ya Waislamu, Swala ya Tarawih yasitishwa
Mar 02, 2025 03:59Baraza Kuu la Waislamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeamua kusimamisha Swala ya Tarawih katika miji ya mashariki inayokaliwa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
-
Mapigano makali yaripotiwa kandokando ya ikulu ya rais mjini Khartoum, Sudan
Mar 02, 2025 03:45Baadhi ya vyanzo vya ndani vimeripoti kuwa Jeshi la Sudan limefanya mashambulizi makali dhidi ya ngome za wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) mjini Khartoum na kwamba mapigano makali yanashuhudiwa karibu na ikulu ya rais.
-
Ramadhani imeanza na mgogoro wa vita unaendelea nchini Sudan
Mar 01, 2025 23:02Sambamba na kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, Jeshi la Sudan SAF limezidisha mashambulizi ya kuuteka kikamilifu mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, kutoka mikononi mwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Hata hivyo kampeni hiyo inasababisha hasara kubwa hasa kwa watoto wa nchi hiyo. Mapigano hayo yamesambaratisha maisha ya vijana na kushadidisha njaa, mbali na janga la majeruhi, wajane na mayatima.
-
Kipindupindu chaua zaidi ya watu 200 nchini Angola
Mar 01, 2025 23:00Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mripuko wa hivi karibuni wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Angola imeongezeka na kupindukia 200.
-
UN yawashutumu viongozi wa Sudan Kusini kwa kuchochea ghasia, machafuko
Mar 01, 2025 09:01Umoja wa Mataifa umesema viongozi wa Sudan Kusini wanaendelea kuchochea ghasia na ukosefu wa amani nchini humo, huku mivutano ya kuwania madaraka, ufisadi na migawanyiko ya kikabila ikiendelea.
-
Zaidi ya wakimbizi 60,000 kutoka DRC wawasili Burundi, wengi ni wanawake na watoto
Mar 01, 2025 07:36zaidi ya watu 60,000 wamevuka mpaka na kuingia Burundi Katika muda wa wiki mbili tu, wakikimbia ghasia na machafuko makubwa yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
-
WFP yasimamisha usambazaji wa chakula Darfur Kaskazini, Sudan
Mar 01, 2025 03:44Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesitisha usambazaji wa chakula cha msaada katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan kutokana na kushtadi mapigano kati ya jeshi la serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).