-
Watu wasiopungua 39 wauawa katika mashambulizi ya waasi nchini Niger
Dec 15, 2024 07:24Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa watu wasiopungua 39 wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha magharibi mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Burkina Faso.
-
Mali, Burkina Faso na Niger zaondoa visa kwa raia wa nchi za ECOWAS
Dec 15, 2024 06:02Mali, Burkina Faso na Niger zimetangaza kuwa zimekuwa "eneo lisilo na visa kwa raia wote" wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), katika mkesha wa mkutano wa kilele wa shirika hilo la kikanda.
-
Jumuiya ya SADC yakabidhiwa rasmi jengo jipya la Makao Makuu yake nchini Botswana
Dec 14, 2024 23:35Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye ndiye mwenyekiti wa hivi sasa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais Duma Boko wa Botswana wamewawakilisha viongozi wengine wa jumuiya na kupokea rasmi jengo la Makao Makuu ya SADC huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana.
-
42 wauawa katika mripuko wa bomu la ardhini katikati mwa Sudan
Dec 14, 2024 23:35Takriban watu 42 wameuawa katika mripuko wa bomu la kutegwa ardhini kwenye Jimbo la Sinnar la katikati mwa Sudan. Vikundi vya kujitolea vinakituhumu Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuhusika na shambulio hilo.
-
Wagombea wa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika washiriki katika mjadala
Dec 14, 2024 08:57Wanasiasa watatu wa Kiafrika wanaotaka kuongoza Tume ya Umoja wa Afrika Ijumaa walishiriki katika mjadala ambapo walieleza kwa kina mipango yao kwa ajili ya usalama wa kikanda huku wakitetea vikali biashara baina ya nchi Afrika miongoni mwa masuala mengine.
-
Raia wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel dhidi ya Gaza
Dec 14, 2024 08:53Maelfu ya raia wa Morocco wameshirikki katika maandamano ya mshikamano siku ya Ijumaa kuunga mkono Wapalestina Gaza ambao wamekuwa wakikabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja.
-
NGO' zalaani ukiukwaji wa haki za binadamu katika mradi wa bomba la mafuta la Uganda -Tanzania
Dec 13, 2024 09:19Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yanadai kuwepo "ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu" karibu na mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta unaojengwa nchini Uganda na Tanzania na kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies ikishirikiana na kampuni ya Uchina ya CNOOC.
-
BBC yatimiuliwa Niger kwa kueneza habari feki
Dec 13, 2024 06:29Serikali ya Niger imetangaza kusimamisha kwa muda wa miezi mitatu matangazo ya redio ya BBC baada ya shirika hilo la serikali ya Uingereza kupatikana na hatia ya kueneza habari feki.
-
AfDB yaongoza kampeni ya ufadhili wa dola bilioni 1.2 wa mradi wa SGR nchini Tanzania
Dec 13, 2024 03:20Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema katika taarifa yake ya hivi karibuni kwamba imetia saini barua ya uratibu wa pamoja baina yake na Benki ya Deutsche na Societe Generale kwa ajili ya kuendesha kampeni yakukusanya hadi dola bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendesha mradi wa reli ya Tanzania kwa kiwango cha SGR.
-
Afrika Kusini yafungua tena kivuko cha mpakani na Msumbiji
Dec 13, 2024 03:18Mamlaka ya Kusimamia Mipaka ya Afrika Kusini (BMA) imetangaza kuwa, harakati za wasafiri katika kivuko kikuu cha mpaka wa Afrika Kusini na Msumbiji sasa ziko wazi hadi litakapotolewa tangazo jingine.