BBC yatimiuliwa Niger kwa kueneza habari feki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120088-bbc_yatimiuliwa_niger_kwa_kueneza_habari_feki
Serikali ya Niger imetangaza kusimamisha kwa muda wa miezi mitatu matangazo ya redio ya BBC baada ya shirika hilo la serikali ya Uingereza kupatikana na hatia ya kueneza habari feki.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 13, 2024 06:29 UTC
  • BBC yatimiuliwa Niger kwa kueneza habari feki

Serikali ya Niger imetangaza kusimamisha kwa muda wa miezi mitatu matangazo ya redio ya BBC baada ya shirika hilo la serikali ya Uingereza kupatikana na hatia ya kueneza habari feki.

BBC imetuhumiwa  kwa kusambaza "taarifa potofu zinazoweza kuyumbisha amani ya kijamii na kudhoofisha ari ya wanajeshi" katika mapambano yanayoendelea nchini humo dhidi ya magaidi wakufurishaji.

Taarifa ya kusitishwa matangazo ya Idhaa ya BBC nchini Niger imetangazwa na Waziri wa Mawasiliano Sidi Mohamed Raliou.

Serikali ya Niger imesema matangazo ya BBC yanatishia utulivu wa kitaifa.

Niger pia huko nyuma iliwahi kusitisha matangaza ya Idhaa ya Ufaransa ya RFI na Televisehni ya Ufaransa ya France 24 kwa kurusha matangazo yanayokiuka sheria za nchi hiyo.