Raia wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel dhidi ya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120134-raia_wa_morocco_waandamana_kulaani_jinai_za_israel_dhidi_ya_gaza
Maelfu ya raia wa Morocco wameshirikki katika maandamano ya mshikamano siku ya Ijumaa kuunga mkono Wapalestina Gaza ambao wamekuwa wakikabiliwa na  mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja.
(last modified 2024-12-14T08:53:28+00:00 )
Dec 14, 2024 08:53 UTC
  • Raia wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel dhidi ya Gaza

Maelfu ya raia wa Morocco wameshirikki katika maandamano ya mshikamano siku ya Ijumaa kuunga mkono Wapalestina Gaza ambao wamekuwa wakikabiliwa na  mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maandamano hayo, yaliyoandaliwa na Tume ya Morocco ya Kutetea Haki za kote katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Maandamano hayo yalikuwa ya 62 katika mfululizo wa maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika nchini humo chini ya kauli mbiu "Gaza ni Amana, Kuanzisha Uhusiano na Israel ni Usaliti."

Waandamanaji wamelaani mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya raia wa Palestina na kukosoa jumuiya ya kimataifa kutoweza kukomesha ukiukaji huo, kwa mujibu wa ripota wa Anadolu.

Aidha walitoa nara kama vile "Wamorocco Wanaunga Mkono Palestina Huru," "Palestina Ni ya Walio Huru," na "Uhusiano na Israel ni Doa la Aibu."

Mnamo Desemba 2020, Morocco na Israel zilitangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya kusimamishwa mwaka 2000 kufuatia kuzuka kwa Intifadha ya pili ya Palestina.

Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kukubali kurejesha uhusiano na Israel mwaka 2020 baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan. Wananchi wa Morocco wamejiunga na wenzao katika nchi za Kiarabu kupinga vikali uamuzi wa serikali zao kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel na wametaka mapatano ya kuanzisha uhusiano huo yafutwe.

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya takriban Wapalestina 45,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, tangu Oktoba 7 2024.

Mwezi uliopita Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa zamani wa vita Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu huko Gaza.

Israel pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa vita vyake dhidi ya Gaza.