-
Uhusiano wa biashara ya mifugo baina ya Ethiopia na Djibouti waimarika baada ya kuzinduliwa reli
Sep 24, 2024 03:59Reli ya Ethiopia-Djibouti jana Jumatatu ilianza kusafirisha mifugo kutoka katikati mwa Ethiopia hadi bandarini nchini Djibouti ikiwa ni ishara ya kuzidi kuimarika uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili jirani za Pembe ya Afrika.
-
Rais Ruto wa Kenya atoa wito wa kufanyika mageuzi katika Umoja wa Mataifa
Sep 23, 2024 08:22Rais William Ruto wa Kenya ametoa wito wa kuwepo mageuzi katika Umoja wa Mataifa ili nchi za Afrika ziweze kupata uwakilishi unaostahiki katika taasisi hiyo muhimu ya dunia.
-
Maelfu ya wakimbizi wa Kiafrika warejea makwao baada ya kuishi Malawi kwa miongo kadhaa
Sep 23, 2024 08:13Makumi ya wakimbizi na watafuta hifadhi kutoka nchi za Kiafrika zilizoathiriwa na vita ambao walikuwa wakiishi Malawi kwa miongo kadhaa sasa wanarejea katika nchi zao kutokana na mpango wa hiari wa serikali unaotekelezwa na serikali ya Malawi pamoja na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ili kuwarejesha makwao wakimbizi.
-
Maandamano yafanyika kote Morocco kuunga mkono Wapalestina
Sep 22, 2024 23:23Zaidi ya maandamano 100 yaliandaliwa kote Morocco siku ya Ijumaa kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza na kuonyesha uungaji mkono kwa Wapalestina wanaodhulumiwa.
-
Mafuriko yaua zaidi ya watu 500 nchini Chad
Sep 22, 2024 23:23Zaidi ya watu 500 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Chad kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini humo.
-
Mtoto wa Museveni: Uganda haitaongozwa na rais ambaye ni raia
Sep 22, 2024 09:21Mkuu wa jeshi la Uganda, ambaye ni mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kwamba, hakuna raia atakayeongoza Uganda na kwamba hilo ni jukumu la wanajeshi au polisi.
-
Maandamano yafanyika Somalia kupinga wanajeshi wa Misri
Sep 22, 2024 08:47Hatua ya Somalia ya kuwaalika wanajeshi wa Misri katika ardhi yake imeibua hitilafu kati ya serikali kuu ya Mogadishu na majimbo yake ya shirikisho, katika kile kinachoweza kuharibu mwelekeo wa nchi hiyo katika mahitaji ya usalama.
-
Chad yakanusha taarifa kuhusu kurejeshwa askari wa Marekani nchini humo
Sep 22, 2024 08:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Abderaman Koulamallah amekanusha madai ya Jenerali wa Marekani Kenneth Eckman wa Kamandi ya Kijeshi ya Marekani Afrika (AFRICOM) kuhusu kurejea wanajeshi wa Marekani nchini mwake, kwa madai kuwa ni kwa ombi la N'Djamena.
-
Guterres asikitishwa pakubwa na hali ya mambo ya al Fasher; Sudan
Sep 22, 2024 04:24Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa "amesikitishwa sana" na ripoti za mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa al Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur, Kaskazini mwa Sudan. Haya yameelezwa na Msemaji wa Antonio Guterres, Stephane Dujarric.
-
UNICEF yataka dola milioni 58.8 kukomesha mlipuko wa mpox Afrika
Sep 21, 2024 23:28Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF), umetoa ombi la dharura la karibu dola milioni 59 kusaidia juhudi za kukomesha maradhi ya MPOX.