-
Magaidi 19 wa al-Shabaab wauawa katika mashambulizi ya anga Somalia
Sep 04, 2024 23:26Wanachama wasiopungua 19 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Somalia katika maeneo ya Shabelle ya Kati na Galgadud.
-
Sudan Kusini: Mahakama ya Kijeshi yawahukumu vifungo jela wanajeshi wanane kwa hatia ya mauaji, ubakaji
Sep 04, 2024 10:51Mahakama ya Kijeshi ya Marid nchini Sudan Kusini imewahukumu wanajeshi wanane kwa mauaji na makosa mengine.
-
Namibia yagawa nyama za wanyamapori kwa watu wanaotaabika kwa njaa
Sep 04, 2024 09:50Serikali ya Namibia imeanzisha mpango wa aina yake wa kukabiliana na njaa wa kuwinda wanyamapori na kugawa nyama kwa wananchi wanaotaabika kwa njaa.
-
China, Tanzania na Zambia zasaini makubaliano mradi wa reli
Sep 04, 2024 09:21Rais Xi-Jinping pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenzao wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba wa maelewano kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari.
-
Boko Haram waua wanakijiji 127, wachoma moto maduka na nyumba kaskazini ya Nigeria
Sep 03, 2024 23:12Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa ni wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamevamia kijiji cha kaskazini mashariki mwa Nigeria wakiwa na pikipiki na kufyatua risasi sokoni na kuteketeza maduka na nyumba sambamba na kuua watu wapatao 127. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International na Polisi ya Nigeria.
-
Ufisadi Serikalini unawafanya vijana wengi wa Kiafrika wahajiri na kukimbilia Ughaibuni
Sep 03, 2024 23:09Karibu asilimia 60 ya vijana wa Kiafrika wanataka kuzihama nchi zao kwa sababu serikali zao hazishikiki kwa ufisadi. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa kwa vijana katika mataifa 16 ya Afrika.
-
Wafungwa 129 wauawa wakijaribu kutoroka jela DRC
Sep 03, 2024 07:58Kwa akali watu 129 wamethibitishwa kuawa na wengine 59 kujeruhiwa wakati wa jaribio la kutoroka jela katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
IOM: Tumeokoa wahamiaji haramu 979 katika pwani ya Libya wiki iliyopita
Sep 03, 2024 03:15Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilitangaza jana Jumatatu kuwa, wahamiaji 979 wameokolewa na kurudishwa nchini Libya katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
-
Lugha ya Kirusi yaanza kufundishwa bure nchini Niger, pigo kwa Kifaransa
Sep 03, 2024 03:14Masomo ya bure ya lugha ya Kirusi yalizinduliwa rasmi jana Jumatatu katika Jumba la lugha ya Kirusi huko Niamey, mji mkuu wa Niger na kuvutia idadi kubwa ya wanafunzi. Hii ni ishara ya kupigwa teke lugha za nchi za Magharibi hasa Kifaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Ikumbukwe kuwa Niger ni nchi ambayo Ufaransa ilikuwa inajifaragua inavyotaka ndani yake.
-
Walioshiriki maandamano dhidi ya serikali Nigeria wafunguliwa mashtaka ya uhaini
Sep 03, 2024 01:06Nigeria siku ya Jumatatu iliwafungulia mashtaka ya uhaini watu 10 walioshiriki katika maandamano ya kuipinga serikali yaliyofanyika nchi nzima mwezi uliopita.