China, Tanzania na Zambia zasaini makubaliano mradi wa reli
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115996-china_tanzania_na_zambia_zasaini_makubaliano_mradi_wa_reli
Rais Xi-Jinping pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenzao wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba wa maelewano kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari.
(last modified 2024-09-04T09:21:29+00:00 )
Sep 04, 2024 09:21 UTC
  • China, Tanzania na Zambia zasaini makubaliano mradi wa reli

Rais Xi-Jinping pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenzao wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba wa maelewano kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari.

Habari zaidii kutoka Beijing zinasema, China, Jamhurii ya Muungano wa Tanzania na Zambia zimesaini makubaliano ya mwanzo kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari katika kanda ya Afrika Mashariki.

Rais Xi-Jinping pamoja na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema wamesaini mkataba huo wa maelewano mjini Beijing ambako viongozi hao wanashiriki mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika ulioanza rasmi leo.

China imesema, iko tayari kuutazama mkutano huo kama fursa ya kupiga hatua mpya ya kufufua ushirikiano wa reli kati ya Tanzania na Zambia ili kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari kwenye kanda hiyo.

Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Rais wa China Xi Jinping

 

Mwanzoni mwa mwaka huu Benki ya Dunia iliidhinisha dola milioni 270 za kusaidia kuimarisha usafiri wa reli kati ya mataifa hayo jirani ya Tanzania na Zambia kunyanyua biashara kwenye eneo hilo.

Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCACA) uulianza rasmi leo huko China utajadili kwa kina ushirikiano mpya wa kiuchumi, maendeleo ya miundombinu na ushirikiano wa pande mbili. Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kuharakisha mabadiliko kunaiingiza dunia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko.