Wanajeshi wa Kizayuni nchini Lebanon: Hatuna chaguo ila kukimbia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i138286-wanajeshi_wa_kizayuni_nchini_lebanon_hatuna_chaguo_ila_kukimbia
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kushindwa jeshi la utawala wa vamizi wa Israel kukabiliana na ndege zisizo na rubani za harakati ya Hizbullah.
(last modified 2026-05-10T11:21:40+00:00 )
May 10, 2026 10:32 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wakimbia Lebanon
    Wanajeshi wa Israel wakimbia Lebanon

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimekiri kushindwa jeshi la utawala wa vamizi wa Israel kukabiliana na ndege zisizo na rubani za harakati ya Hizbullah.

Wanajeshi wa utawala vamizi walioko kusini mwa Lebanon wamekiri kwamba wametumia mbinu za mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nyavu za uvuvi, ili kujilinda dhidi ya ndege zisizo na rubani za Hizbullah, bila mafanikio.

Wameongeza kuwa kwa njia hizo wanajaribu kupunguza athari za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Hizbulah. Mmoja wa wanajeshi wa Israel, ambaye amekuwa Lebanon kwa mara ya sita, amesema kwamba Wazayuni wanakabiliwa na tishio la mara kwa mara. Hawana njia ya kukabiliana na ndege hizi zisizo na rubani isipokuwa kukimbilia mafichoni.

Askari huyo ameongeza kuwa ving'ora vya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Hizbullah husikika mara kadhaa wakati wa mchana, na sauti ya ndege mpya zisizo na rubani za harakati hiyo inasikika kwa tabu sana.

Askari huyo amesema, licha ya madai yaliyotolewa kuhusu kupatikana suluhisho za kiufundi dhidi ya ndege hizo zisizo na rubani, hakuna mifumo ya kiisasa ya au zana bora za kukabiliana nazo.