Ramaphosa: Hujuma dhidi ya wageni haziakisi maoni ya Afrika Kusini
-
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anasema kuwa "wafursa" walipanga mashambulizi dhidi ya wahamiaji dhidi ya wageni huku akitaka kuzihakikishia nchi nyingine za Afrika, ambazo zimeelezea wasiwasi wake kuhusu raia wao.
"Lazima tuweke wazi kuwa hakuna nafasi nchini Afrika Kusini kwa chuki dhidi ya wageni, mivutano ya kikabila, kutovumiliana au kuibua machafuko", amesema Rais Cyril Ramaphosa katika barua ya wazi iliyotolewa na ofisi yake siku ya Jumatatu .

Maandamano mtawalia na hatua za mabavu dhidi ya wahamiaji zimeshuhudiwa katika wiki za karibuni nchini Afrika Kusini hatua ambazo zimelaaniwa na kukemewa vikali na nchi mbali zikiwemo Nigeria na Ghana.
Nigeria wiki iliyopita ilieleza kuwa itawarejesha nyumbani raia wake wapatao 130.
Rais wa Afrika Kusini amesema kuwa vitendo vya mabavu na uhalifu wa vilivyowalenga raia wa kigeni hivi karibun katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo haviwakilishi maoni na mitazamo ya wananchi wa Afrika Kusini wala kuakisi sera za serikali ya nchi hiyosi sera za serikali ya nchi hiyo.