-
Eneo la mashariki mwa DRC laendelea kuteseka kwa wimbi jipya la mahambulizi ya waasi wa ADF, M23
Aug 04, 2024 03:52Wimbi la mashambulizi mapya ya waasi wa ADF na M23 linaedelea kuwatesa wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku mapigano baina ya wanajeshi wa serikali na waasi wa makundi hayo mawili yakiendelea.
-
Takriban watu 23 wameuawa katika shambulizi la RSF huko El Fasher nchini Sudan
Aug 04, 2024 03:51Takriban watu 23 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la mizinga lililofanywa na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini.
-
UN yataka kuongezwa juhudi za kupeleka msaada wa haraka kwa waliokumbwa na njaa Sudan
Aug 03, 2024 23:03Kaimu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya misaada amesema kuwa, janga la njaa katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan ni ukumbusho mzito wa wajibu wa jumuiya ya kimataifa kupeleka misaada ya kuokoa maisha mara moja.
-
Polisi: Watu 32 wauawa katika shambulio Somalia
Aug 03, 2024 10:05Kwa akali watu 32 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga na watu wenye silaha kulenga eneo maarufu la ufukweni katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Malawi yachapisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025
Aug 03, 2024 07:22Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) jana Ijumaa ilichapisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao umepangwa kufanyika Septemba 16, 2025. Ratiba hiyo imetangazwa huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi.
-
Kambi ya upinzani Tunisia yalaani 'mbinyo' wa kabla ya uchaguzi wa rais
Aug 03, 2024 03:24Wagombea urais wa kambi ya upinzani nchini Tunisia, mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyama vya kisiasa vimelaani 'vizuizi vya kiholela' vilivyowekwa dhidi yao na serikali ya Tunis kabla ya uchaguzi wa Oktoba 6.
-
UN: Eneo la Darfur Kaskazini nchini Sudan limekumbwa na baa la njaa
Aug 03, 2024 00:56Hatimaye imedhihirika kuwa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan linasumbuliwa na baa la njaa, imesema Kamati ya Tathmini ya Njaa inayohusisha mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau.
-
Hujuma ya kigaidi hotelini Mogadishu, watu kadhaa waripotiwa kuuawa
Aug 03, 2024 00:56Mlipuko na milio ya risasi imetikisa hoteli karibu na ufuo wa bahari katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu huku watu kadhaa wakiripotiwa kupoteza maisha.
-
Watu watatu wameuawa nchini Nigeria katika maandamano ya kupinga gharama kubwa ya maisha
Aug 02, 2024 09:08Takriban waandamanaji watatu wameuawa katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria siku ya Alhamisi, katika maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha na utawala mbovu.
-
Benki ya Dunia yaipa Somalia dola milioni 125 za bima ya ukame
Aug 02, 2024 03:08Benki ya Dunia imeidhinisha dola milioni 125 kwa ajili ya kuisaidia Somalia kuanzisha bima ya maafa ya ukame kwa wafugaji 180,000 wakiwemo wanawake 90,000.