-
Mawaziri wa Rwanda, Burundi na DRC kukutana kujadili mzozo wa kidiplomasia
Jul 10, 2024 03:35Mawaziri wa Rwanda, Jamhurii ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi wamekubaliana kukutana kujadili mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi zao ambao umetishia usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
-
Umoja wa Mataifa: Uganda ilitoa msaada kwa waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Jul 09, 2024 23:00Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kwamba, jeeshi la Uganda limetoa msaada kwa waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Rais William Ruto atia saini muswada wa IEBC, mashinikizo ya Gen Z yaanza kuzaa matunda
Jul 09, 2024 07:30Rais William Ruto wa Kenya Jumanne ya leo ametia saini muswada uliorekebishwa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka wa 2024 kuwa sheria.
-
Mahakama Kenya yailaumu polisi kwa kifo cha mwandishi habari wa Pakistan
Jul 09, 2024 04:12Mahakama nchini Kenya jana ilitoa uamuzi ikisema kuwa kitendo cha polisi wa nchi hiyo cha kumpiga risasi mwandishi wa habari wa Pakistan mjini Nairobi mwaka 2022 kilikuwa kinyume cha sheria na kinyume na katiba.
-
Rwanda: Tumezingatia nia ya Uingereza ya kusitisha mpango tata wa uhamiaji
Jul 09, 2024 04:05Rwanda jana ilisema kuwa imetilia maanani nia ya serikali ya Uingereza ya kusimamisha mpango tata wa uhamiaji ambao ulisainiwa na nchi mbili hizo kwa lengo la kuwazuia wahamiaji haramu kuingia Uingereza kupitia mfereji wa maji unaozitenganisha nchi mbili za Uingereza na Ufaransa kwa kutumia boti ndogo za usafiri.
-
Ripoti ya UN: Wanajeshi wa Rwanda wanapigana pamoja na waasi wa M23 huko Kongo
Jul 08, 2024 22:56Ripoti ya karibuni iya Umoja wa Mataifa imefichua kuwa kati ya wanajeshi 3,000 hadi 4,000 wa Rwanda wanapigana bega kwa bega na waasi wa kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku Kigali ikiongoza pakubwa oparesheni za kundi hilo.
-
Ecowas yamteuwa Rais wa Senegal kuzungumza na Burkina Faso, Mali na Niger
Jul 08, 2024 22:54Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imemtaka Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye kushirikiana na nchi tatu wanachama wake wa zamani zinazoongozwa kijeshi kujaribu kuliunganisha eneo hilo ambalo utulivu wake umekuwa hatarini tangu zilipoamua kujitoa katika jumuiya hiyo mwezi Januari mwaka huu.
-
Wanajeshi wa Marekani waanza kuondoka Niger baada ya kutimuliwa, Wajerumani wanafuatia
Jul 08, 2024 07:13Marekani imeanza kuondoa askari wake wote na zana zake za kijeshi huko Niger baada ya kutimuliwa kutokana na siasa zao za kibeberu. Kuondoka wanajeshi hao kumekuja kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 15 waliyopewa na serikali ya Niamey ya kwamba hawatakiwi kuonekana tena kwenye ardhi ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Rais wa Nigeria ateuliwa tena kuwa mwenyekiti wa ECOWAS, ahimiza umoja
Jul 08, 2024 07:11Rais Bola Tinubu wa Nigeria ametoa mwito kwa viongozi wa nchi za magharibi mwa Afrika kushikamana na kufanya kazi kwa pamoja ili kudumisha kikosi cha kikanda cha kukabiliana na matishio ya usalama yanayozidi kuongezeka katika eneo hilo.
-
Mashahidi wa mauaji ya halaiki Shakahola kuanza kutoa ushahidi leo huko Kenya
Jul 08, 2024 03:52Kesi ya mauaji ya Msitu wa Shakahola inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo mahakamani wakati mashahidi watakapotoa ushahidi wao dhidi ya mshukiwa mkuu wa mauaji hayo, mchungaji Paul Mackenzie, na wenzake 93.