Mawaziri wa Rwanda, Burundi na DRC kukutana kujadili mzozo wa kidiplomasia
Mawaziri wa Rwanda, Jamhurii ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi wamekubaliana kukutana kujadili mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi zao ambao umetishia usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Uamuzi huuo umefikiwa baada ya kukamilika kwa kongamano la siku tatu nchini Tanzania la mawaziri kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ambapo walijadili usalama wa kikanda.
Wakati wa kongamano hilo, mawaziri hao walijadili hali ya mahusiano baina ya nchi na athari mbaya katika ajenda ya utangamano na kuzihimiza nchi washirika kutumia mifumo iliyopo kutatua migogoro baina yao.
Uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa umezorota kutokana na vita baina ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasiai ya Congo na waasi wa M23 mashariki mwa taifa hilo huku serikali ya Congo ikilaumu Rwanda kwa kufadhili wanamgambo hao.
Hata hivyo hakuna tarehe iliyoafikiwa kwa ajili ya mkutano huo.
Wajumbe wa Rais na mawaziri kutoka nchi hizo walikutana awali kupîtia kwa juhudi za upatanishi za Umoja wa Afrika zinazoongozwa na Angola lakini suluhu haikuafikiwa.
Licha ya hayo, hiii itakuwa mara ya kwanza kwa mawaziri kutoka Burundi kukutana na wenzao wa Rwanda kabla ya mwisho wa mwezi Oktoba mwaka huu baada ya Bujumbura kuituhumu Kigali kwamba, ilihusika na shambulio la kigaidi nchini humo. Burundi ilikanusha kuhusika na tukio hilo na ikachukua uamuzi wa kufunga mpaka wake na Rwanda.