-
Waguinea Bissau waandamana kulaani mapinduzi, viongozi wa kanda wakutana kutafuta suluhisho
Dec 13, 2025 22:37Mamia kadhaa ya watu wameingia barabarani katika mji mkuu wa Guinea-Bissau, Bissau kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita viongozi wa upinzani wanaoshikiliwa waachiliwe huru, huku viongozi wa kikanda wakijiandaa kukutana leo Jumapili kujadili namna ya kuupatia suluhisho mgogoro huo.
-
Serikali ya Kongo yatoa hakikisho; yasema haitasalimu amri licha ya hali ya wasiwasi mashariki mwa nchi
Dec 13, 2025 06:22Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Ijumaa ilitoa hakikisho ikieleza kuwa jeshi la nchi hiyo halitasalimu amri" kufuatia kutekwa mji wa Uvira.
-
UN yasikitishwa na shambulio la droni lililoua zaidi ya raia 30 Sudan
Dec 13, 2025 05:23Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesikitishwa sana na shambulio la droni yaani ndege isiyo na rubani lililoua raia wasiopungua 30 katika Jimbo la Darfur Kusini, huko Sudan.
-
WFP yaamua kupunguza mgao wa chakula kwa wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan
Dec 13, 2025 03:53Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kwamba litaanza kupunguza mgao wa chakula unaotolewa kwa watu wa Sudan wanaokabiliwa na hatari ya njaa, kutokana na ukosefu wa ufadhili.
-
Kama ishara ya mvutano na Ethiopia: Eritrea yajiondoa tena katika jumuiya ya IGAD
Dec 13, 2025 03:03Eritrea ilitangaza jana Ijumaa kwamba imejiondoa katika Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali za nchi za Afrika Mashariki, maarufu kama IGAD, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akielezea wasiwasi wake kuhusu mvutano kati ya Asmara na Addis Ababa.
-
Mamia ya askari wa Afrika Magharibi wanaendelea 'kusafisha' Benin
Dec 12, 2025 23:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin amesema wanajeshi wapatao 200 wa Afrika Magharibi, wengi wao kutoka Nigeria na Ivory Coast, wako nchini Benin kuiunga mkono serikali kufuatia mapinduzi yaliyofeli Jumapili iliyopita.
-
Mvua kubwa na radi yaua watu 14 nchini Malawi
Dec 12, 2025 23:02Radi imeua watu 14 nchini Malawi katika muda wa wiki mbili zilizopita, huku nyumba 8,000 zikiharibiwa na kubomoka katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika kufuatia kushtadi mvua kubwa nchini humo.
-
RSF yatuhumiwa kuhusika na mengi ya matukio 1,300 ya ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Dec 12, 2025 06:44Shirika moja la kutetea haki za wanawake limesema, limerekodi matukio yapatayo 1,300 ya vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vilivyofanywa katika vita vya ndani nchini Sudan huku Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kikishutumiwa kuhusika na akthari ya vitendo hivyo.
-
Benki Kuu ya Ufaransa yahusishwa na mauaji ya kimbari ya Watutsi ya 1994 nchini Rwanda
Dec 12, 2025 06:41Wanaharakati wa haki za kibinadamu na watafiti mbalimbali wameituhumu Benki Kuu ya Ufaransa kwamba ilihusika kwa namna moja katika matukio yaliyopelekea kutokea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda dhidi ya jamii ya Watutsi.
-
Rais Samia apokea hati za utambulisho za balozi wa Iran nchini Tanzania
Dec 12, 2025 03:28Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana alipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.