-
UNHCR yahimiza jamii ya kimataifa kuwasaidia wakimbizi wa Sudan nchini Chad
Nov 08, 2025 23:09Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetoa mwito wa dharura wa kusaidiwa sana kimataifa maelfu ya watu waliokimbilia Chad kukwepa mauaji ya kimbari nchini Sudan. Wasudan wanaendelea kumiminika katika nchi jirani ya Chad kutoka eneo la Darfur la magharibi mwa Sidan.
-
Wamorocco waandamana kuunga mkono Palestina na kulaani mzingiro Gaza
Nov 08, 2025 07:02Maelfu ya wananchi wa Morocco wameingia mitaani na kushiriki maandamano ya kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, sanjari na kulaani mzingiro dhidi ya Gaza na njama za Israel za kukwamisha upelekaji misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.
-
AU yatoa wito wa kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala Nigeria, yapinga vitisho vya Trump
Nov 08, 2025 04:28Tume ya Umoja wa Afrika imeelezea wasiwasi wake kuhusu kauli za hivi karibuni za Marekani, ambazo zimeituhumu serikali ya Nigeria kuwa inashiriki katika mauaji iliyodai kuwa yanayowalenga Wakristo, na kudokeza uwezekano wa kuingilia kijeshi kwa kisingizio cha "kutetea uhuru wa kidini."
-
Ghannouchi na wanaharakati wa kisiasa wagoma kula kuonyesha mshikamano na Ben Mbarek
Nov 08, 2025 04:27Timu ya utetezi ya Rached Ghannouchi, spika wa zamani wa Bunge la Tunisia na mkuu wa harakati ya Ennahda, ilitangaza jana Ijumaa kwamba mwanasiasa huyo mkongwe ameanza mgomo wa kula usio na kikomo kuonyesha mshikamano na Jaouhar Ben Mbarek, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kundi la National Salvation Front and Citizens Against the Coup linalompinga Rais wa Tunisia, Kais Saied.
-
Balozi wa Russia nchini Sudan: Mamluki wa Ukraine wanaendeshaji droni huko Darfur
Nov 08, 2025 03:45Balozi wa Russia nchini Sudan, Andrey Chernovol, ameripoti kwamba kuna uvumi unaosambaa nchini Sudan kuhusu uwepo wa Waukreini wanasimamia operesheni za ndege zisizo na rubani katika safu ya waasi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Mahakama ya ICC yathibitisha mashtaka dhidi ya Joseph Kony
Nov 08, 2025 00:40Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi wamethibitisha kuwa kiongozi wa waasi wa Uganda Joseph Kony anakabiliwa na mashtaka ya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu na hivyo kufungua njia kwa ajili kuanza kesi yake iwapo tu atatiwa nguvuni.
-
Jeshi la Sudan lakabiliana na mashambulizi ya droni katika mji mkuu Khartoum
Nov 08, 2025 00:38Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kikosi chake cha ulinzi wa anga jana Ijumaa kilinasa kundi la ndege zisizo na rubani (droni) zilizokusudia kufanya mashambulizi katika mji wa Omdurman, magharibi mwa Khartoum, na katika mji wa kaskazini wa Atbara.
-
Watu 145 washtakiwa kwa uhaini wakidaiwa kuhusika katika maandamano ya vurugu Tanzania
Nov 08, 2025 00:37Waendesha mashtaka nchini Tanzania jana Ijumaa wamewashtaki takriban watu 145 kwa kosa la uhaini madai ya kuhusika katika maandamano ya vurugu yaliyozuka wakati wa uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na Reuters.
-
Kenya yataka majibu kwa Tanzania kuhusu raia wake waliokumbwa na misukosuko ya baada ya uchaguzi
Nov 07, 2025 08:21Kenya imeitaka Tanzania itoe majibu kuhusu hali ya raia wake waliojipata kwenye mzozo wa baada ya uchaguzi, huku ikishinikiza serikali ya nchi hiyo ihakikishe usalama wao na kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa haki zao.
-
Rais mzee zaidi duniani aapishwa kuongoza Cameroon kwa muhula wa nane
Nov 07, 2025 03:52Kiongozi wa muda mrefu wa Cameroon, Paul Biya, ameapishwa kwa muhula mpya wa miaka saba kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita, ambao mpinzani wake ameutaja kama "mapinduzi ya kikatiba".