-
Udiplomasiia amilifu wa Iran na Uturuki
Jun 20, 2019 03:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu leo Alkhamisi amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake wa Iran, muhammad javad Zarif katika mji wa Isfahan ambako pande hizo mbili zimejadili masuala ya pande mbili na kikanda.
-
Droni ya ujasusi ya Marekani yatunguliwa katika pwani ya kusini mwa Iran
Jun 20, 2019 03:11Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kutungua drone au ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya Marekani ambayo ilikuwa imejipenyeza katika mipaka ya Iran mkoani Hormozgan kusini mwa nchi.
-
Iran: Hatutarefusha muhula wa siku 60 wa EU kufungamana na JCPOA
Jun 19, 2019 08:15Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) amesema muda wa siku 60 ambao Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliupa Umoja wa Ulaya uwe umetekeleza ahadi zake za kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hautarefushwa.
-
Muqawama mbele ya Marekani; taifa la Iran litapata ushindi katika vita vya irada
Jun 19, 2019 02:58Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mapambano au muqawama ndio njia pekee ya kukabiliana na adui na kuongeza kuwa: "Mapambano ni njia pekee ya kupata ushindi mbele ya sera za Marekani, na ushindi wa taifa la Iran uko karibu."
-
Iran yafungua kituo kikubwa zaidi cha kutengeneza dawa Asia Magharibi
Jun 18, 2019 22:12Kituo kikubwa zaidi cha kutengeneza dawa Asia Magharibi kimefunguliwa Jumanne katika mkoa wa Alborz magharibi mwa Tehran sambamba na kuzinduliwa dawa mpya katika kituo hicho.
-
Shamkhani: Siasa za ugaidi mamboleo za Marekani zimelenga utambulisho wa nchi mbalimbali
Jun 18, 2019 08:51Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa siasa za ugaidi mamboleo za Marekani ambazo zinajumuisha masuala kama nyenzo za intelijinsia, vita vya kisaikojia, hujuma za kimtandao, vita vya kielektroniki, na kuhatarishwa mazingira zinalenga utambulisho na mamlaka ya kitaifa ya nchi mbalimbali duniani.
-
Meja Jenerali Bagheri: Mafuta ya nchi nyingine hayatauzwa nje kwa amani mpaka ya Iran yauzwe
Jun 18, 2019 08:05"Iwapo Iran itataka kuzuia uuzaji nje wa mafuta ya Ghuba ya Uajemi itatangaza suala hilo waiwazi na haitaficha suala hilo na kufanya hadaa kama inavyofanya Marekani na vibaraka wake wa kikanda na kimataifa."
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa taifa la Misri kufuatia kifo cha Mohammad Morsi
Jun 18, 2019 07:58Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa pole kwa familia ya Mohammed Morsi, kufuatia kifo tata cha rais huyo wa zamani wa Misri.
-
Rais Rouhani: Nchi za Ulaya zina muda mfupi wa kuiokoa JCPOA
Jun 17, 2019 08:34Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi za Ulaya zina muda mfupi wa kuyaokoa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran kuongeza mara 4 urutubishaji wa urani, kupitisha kiwango cha kilo 300
Jun 17, 2019 08:12Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia Juni 27 itapitisha kiwango cha urutubishaji wa urani mara nne zaidi, na kwamba akiba yake ya urani itapita kiwango cha kilo 300 kilichoanishwa kwenye makubaliano ya nyuklia kufikia tarehe hiyo.